9/100. Lipa gharama kuanza safari ya ndoto yako.

Habari

Karibu katika mchakamchaka wa kuendeleza changamoto ya siku mia moja, ikiwa leo tupo siku ya nane. Tunaendeleza pia uchambuzi wetu wa the alchemist kilichoandikwa na mwandishi Paulo Coelho. Tujifunze na kuweka katika matendo tunapoelekea katika safari ya mafanikio.

Baada ya mazungumzo ya muda na mzee yule, Santiago alimwona ni mzee mwenye busara na hivyo kuamua kushirikisha ndoto yake kuhusu hazina ya maisha yake. Mzee alimwambia ili amfafanulie basi ni lazima amlipe kwanza.

Alimwambia ampe asilimia 10 ya kondoo wake, Santiago alikubali na mzee yule alimweleza kwamba hazina ya maisha yake ipo kwenye mapiramidi ya misri, hivyo auze kondoo wake na aanze safari ya kuelekea misri.

Santiago alizidi kuchanganyikiwa, ndiyo kitu hicho ambacho mtafsiri wa Kwanza alimweleza. Lakini hakutaka kuamini, ila safari hii alilipa gharama kujua alichokuwa anakijua tayari.

Mzee huyo alimpa nasaha nyingi sana kuhusu umuhimu wa mtu kuchagua kuishi kusudi la maisha yake. Alimweleza safari iyo itakuwa ngumu sana, lakini alimpa neno moja, pale ambapo unataka kitu kweli, dunia nzima itafanya kila namna kuhakikisha unakipata.

Kuna vitu ambavyo tunavijua kwenye maisha, lakini tunavidharau na kuchukulia kawaida, ni mpaka pale tunapolipa gharama ndiyo tunaelewa umuhimu wa kile ambacho tayari tulikuwa tunakijua.

Kitendo cha Santiago kulipa gharama na hata kuuza kondoo wake, kilimsukuma kuanza safari ya kuelekea kwenye hazina yake. Kuna vitu vinakuzuia wewe usianze safari ya kuelekea kwenye ndoto yako. Lazima uwe tayari kulipa gharama ya kupoteza vitu hivyo ili uanze safari ya kuelekea kwenye hazina yako.

DUNIA INA MWONGOZO UNAOTAKA.

Haikuwa rahisi kwa Santiago kufikia maamuzi y kuuza kondoo wake. Lakini baada ya kupata nasaha za yule mzee, alikasirika na kupata matumaini kwa wakati mmoja.

Alipata hasira Kwa nini alimjua yule mzee ambaye alimweleza ukweli kuhusu kusudi lake la maisha, lakini pia alipata matumaini kwamba safari hiyo inawezekana.

Mzee alimweleza kama atajifunza kuelewa lugha ya dunia, basi majibu ya kila kitu ataweza kuyapata. Alimkabidhi mawe mawili moja jeusi na jeupe ambaye alimwambia majina ya mawe hayo ni urim na thummim. Jiwe jeusi inaashiria NDIYO na jiwe jeupe linaashiria HAPANA.

Alimweleza anapokuwa na mashaka au kuwa njia panda na asijue kipi sahihi kufanya, basi alipaswa kuuliza swali na kisha kutoa jiwe mfukoni,likitoka jeusi ni ndiyo na jeupe ni hapana.

Tunajifunza kwamba huhitaji kujua kila kitu kabla hujaanza safari ya ndoto yako, bali unapaswa kuanza, na kadiri unavyokwenda, dunia itakuwa inakupa mwongozo unaotaka.

Usianze kufikiria mambo magumu kabla hata hujaanza, inakubidhi uanze na kisha utakapokutana na ugumu, dunia itakuonesha njia ya kuvuka ugumu huo.

Rafika yangu naamini umepata kitu kitachokusaidia katika safari yako ya mafanikio.

Limeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio na maisha na pia ni mpishi wako.Nakutakia siku njema yenye mafanikio, tukutane kesho majaaliwa.

Maureen Kemei anayekujali sana

Kemeimaureen32@gmail.com

0713698650

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *