Habari
Karibu katika Kuendelea na uchambuzi wa kitabu the alchemist kilichoandikwa na Paulo Coelho.
Santiago alianza safari ya kuelekea Misri ili kufika kwenye mapiramidi ambapo hazina yake ipo. Alifika Misri na hakuwa akijua kuongea kiarabu, hivyo mawasiliano yalikuwa taabu. Alienda kwenye mgahawa na hapo akakutana na kijana ambaye aliweza kuongea lugha yake.
Alifurahi sana kukutana na kijana yule na waliongea mengi, baadaye akamwambia lengo lake la kwenda kwenye mapiramidi. Kijana yule akamuuliza una fedha, maana mapiramidi yako mbali na ni safari ya muda mrefu jangwani.
Santiago akamjibu kwamba fedha anayo, basi kijana akamwambia waongozane kuelekea eneo ambalo watapata taarifa za kuanza safari, na akamuonya kwamba eneo lile watu siyo waaminifu, hivyo ampe fedha zake akae nazo.
Santiago hakuona tatizo kwa kuwa wanaongozana, basi alimpa na kuhakikisha hamwachi muda wote wanakuwa pamoja. Walipita gulioni ambapo palikuwa na watu wengi wakifanya mauzo na manunuzi, Santiago alishangazwa na vitu ambavyo hakuwahi kuviona.
Wakati anashangaa kwa vitu hivyo aligeuka kumwangalia kijana yule na hakumw+ona tena kijana yule, na hapo ndipo aligundua kwamba ametapeliwa.Hili lilimuumiza sana, kondoo ameshauza na kwenye hazina hajafika na hata tena fedha.
Kwenye safari ya kuelekea kwenye ndoto zako, utaibiwa na kutawaliwa utakutana na watu ambao utawaamini kwa ahadi na mipango yao, lakini wataishia kukuangusha na kukuibia chochote ulichonacho.
Unapokutana na hali kama hii jua siyo mwisho wa safari yako, kama ambavyo tutaendelea kijifunza kwa hatua ambazo Santiago alichukua.
Asante Sana kwa kusoma makala hii naamini unajifunza kitu, maana dhumuni yetu hapa ni kujifunza na kufanyia kazi. Nikutakie mafanikio mema.
Makala hii imeandikwa na Kemei Maureen
Mawasiliano :
Email: Kemeimaureen32@gmail.com
0713698650