18/100.Tabia zinazowafisha watu kwenye mafanikio.

Habari
Nikukaribishe Mwana mafanikio leo tunaangazia kitabu cha ;High performance habits,how extraordinary people become that way ambacho kimeandikwa na kocha wa mafanikio Brendon Burchard.

KANUNI ZA ZAMANI HAZIFANYI KAZI.
Watu wengi wamekuwa wakijifunza kanuni hizo za mafanikio, ambazo zote zimejengwa kwenye msingi wa fanya kazi kwa juhudi, penda sana unachofanya, jitume kuliko wengine, kuwa na shukrani na kuweka mkazo kwenye ubora wako na siyo madhaifu yako.

Kanuni hizo hazifanyi kazi siyo kwa sababu siyo sahihi, ni sahihi sana, na unapokuwa unaanza, kanuni hizo zinakuwezesha kujijengea msingi sahihi.

Lakini kuna hatua unafika,kanuni hizo hazifanyi kazi tena. Hapo ndipo wengi wanapokuwa wamekwama. Kwa sababu wanajua kanuni iliyowafikisha pale walipofika, lakini kadiri wanavyoifanyia kazi haileti tena yale matokeo waliyotegemea kupata.

Mfano wakati mtu anaanza kazi au biashara, kadiri anavyoweka kazi zaidi ndivyo a anapata matokeo mazuri zaidi, na hayo yanamwezesha kukua zaidi.

Lakini anafika hatua fulani ya mafanikio ambayo kadiri anavyoweka kazi zaidi haileti tena matokeo makubwa zaidi.

Hapo ndipo mtu anahitaji vitu vingine ili apige hatua zaidi. Na kinachohitajika katika hatua hii ni tabia ambazo mtu anakuwa nazo.

Watu wengi wamekuwa wanaiishi misingi ya mafanikio, lakini hawajali sana kuhusu tabia zao binafsi.wasichojua ni kwamba, kadiri unavyofanikiwa, ndivyo tabia zako binafsi zinavyokuwa na athari kwenye mafanikio yako.

Hivyo kama umefika hatua ya maisha yako, ambapo umekazana kuiishi misingi ya mafanikio, na mwanzo ilikusaidia ila kwa sasa unaona haikusaidii tena , suluhisho siyo kuacha misingi hiyo, bali suluhisho ni kujijengea tabia bora zaidi.

Unapoishi misingi ya mafanikio, halafu ukajijengea tabia bora, utaweza kufanikiwa sana.

Hatua unazochukua zinaleta matokeo makubwa sana pale ambapo unakuwa na tabia sahihi zinazobeba misingi hiyo.

Tukutane kesho mpendwa ambapo tutajifunza kuhusu tabia hizo tunazopaswa kuwa nazo tukiendelea na safari ya mafanikio.

Makala hii imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio na maisha.

Maureen Kemei
Blog kufikirichanya.wordpress.com

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *