Habari
Karibu Mwana mafanikio leo tukianza kujifunza kutoka kitabu makini sana cha kanuni ya siku ya mafanikio . Ambacho kimeandikwa na kocha wa mafanikio Dr Makirita Amani.
Kocha anatushirikisha kwamba mafanikio haiji tu kwa kustukia, au kufikiria kuamka siku moja kama umetajirika, yaani Kulala masikini na kutarajia kuamka tajiri . Anaeleza kwamba mafanikio huja kwa kuamua kuchukua hatua ndogo ndogo kila siku.
Anaeleza kuwa safari ya elfu moja huwa inaanza na hatua moja zitakapofanyika kwa kurudia rudia ndiyo zinakamilisha safari ya mafanikio.
Kila siku unayoishi ndiyo inachangia kwenye mafanikio yako, anasema kuijua hii ndio ukombozi mkubwa kwenye maisha. Kuliko maarifa yoyote ile.
Wengi ambao hawajafanikiwa wanaisubiri na hata kukosa furaha kwa sababu wanaisubiri siku moja ya mafanikio. Ambayo haipo huku wakipoteza siku nyingi ambazo ndizo zingechangia mafanikio wanayotaka.
Kitu kikubwa ambacho tunapaswa mimi na wewe kuondoka nacho kwenye kitabu hiki makini ni kufahamu kwamba mafanikio ni kila siku.
Badala ya kusubiria siku moja ambayo kwayo utakuwa umepata kila kitu. Ndiyo sasa uanze ufurahie mafanikio yako, unapaswa uanze uishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.
Sababu mkusanyiko wa siku ambazo umeziishi kwa mafanikio ndiyo mafanikio ya maisha yako. Kila siku mambo ya kufanya yanazidi kuongezeka huku muda ukipata ule ule masaa 24.
Kama shughuli za kufanya zinaongezeka kila siku, muda ukipaki ule ule. Kwa hivyo tunajiuliza tunaweza je, kuuishi mafanikio kwenye masaa 24 tuliyonayo kwenye siku yetu?
Ili siku yako iwe ya mafanikio ni muhimu uijue na uwe na kanuni utakayoitumia kuendesha siku yako kwa usahihi.
Tutajifunza namna ya kuvuka kuwa watu wa kufanya mambo kikawaida na kuendesha maisha kwa kubahatisha. Na kujua namna ya kuendesha siku kwa mpangilio maalum, ambayo inatokana na kanuni tunayojitengenezea wenyewe.
Wanaofanikiwa wamekuwa ni watu wa kuamka asubuhi na mapema, wakati bado dunia imelala na kujipatia muda tulivu wa kufanya mambo ya msingi na muhimu kabisa.
Mafanikio ni kila siku, yapaswa kuiheshimu sana kila siku tunayoipata. Kutumia vizuri ili kupata matokeo ya tofauti na bora zaidi. Kurudia rudia hivyo kila siku ili kuwa na mafanikio bora yenye thamani kubwa.
Rafiki, tukutane kesho ili tuzidi kujifunza zaidi kuhusu namna ya kupangilia na kuzifahamu kanuni hizo. Na kutumia ili tupate kuwa washindi kwenye kila siku yetu.
Makala hii imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio, ushauri nasaha na uandishi .
Maureen Kemei
Blog, kufikirichanya.wordpress.com