Karibu
Namshukuru Mungu kwa uhai na zawadi ya siku nyingine ya ushindi. Tunajifunza leo kutoka kitabu cha 21 lessons for the 21st century kimeandikwa na Mwana historia Yuval Noah Harari.
Kwenye kitabu hiki, Yuval amezichambua changamoto kubwa 21 zinazotukabili kwenye karne hii ya 21 na kupendekeza hatua tunazopaswa kuchukua ili tusiachwe nyuma na mabadiliko yanayotokea kwa kasi kubwa.
UWAZI NI NGUVU KUBWA.
Tunaishi kwenye zama ambazo Kuna mafuriko ya taarifa. Yaani maarifa na taarifa ni nyingi mno kiasi kwamba, badala ya maarifa na taarifa hizi kuwa msaada kwetu katika kufanya maamuzi, zinakuwa kikwazo.
Kwa sababu kunapokuwa na maarifa na taarifa nyingi, lakini tukakosa uwazi au tukashindwa au kuzielewa kwa ubaya, tunaishia kubaki katika njia panda tusichukue ni hatua ipi ya kuchukua.
Wingi wa maarifa na taarifa zilizopo, unapelekea hali kubwa ya upinzani baina ya maarifa na taarifa. Taarifa moja inaweza kuwa inakuambia hiki, huku taarifa nyingine ikipingana na hicho cha mwanzo. Katika hali kama hii, ni vigumu sana kujua ni hatua gani ipi uchukue kama huna uwazi ndani yako.
UWAZI ni nguvu kubwa katika karne hii ya mafuriko ya taarifa na maarifa. Uwazi unaanza kwa kujijua wewe mwenyewe na kujua unataka nini kwenye maisha yako. Kisha kuchagua taarifa na maarifa yanayoendana na kile unachotaka na kuachana na mengine.
Ukijua kwamba unachochagua wewe siyo kitachokuwa sahihi kuliko vingine vyote, bali kitakuwa sahihi kwako kulingana na unachotaka kwenye maisha yako.
Upo usemi unaosema ukifa kwa kiu wakati umezungukwa na maji ni ujinga, lakini zama hizi watu wengi wanaangamia kwa kukosa maarifa, huku wanazama kwenye mafuriko ya maarifa.
Nikafahamu kuwa kinachokosekana zama hizi siyo maarifa, bali uwazi. Nimejifunza kwamba napaswa kuwa mwazi kwangu binafsi na kuwa tayari kuchagua kimoja na kuachana vitu vingine.
Jambo hili wachache wanaliweza na naweza kuwa mmoja wao ata na wewe rafiki unayesoma nakala hii. Kujua unayotaka kwenye maisha, kuchagua aina ya maarifa yanayoendana na kile unachotaka na achana na mengine yote.
Tukutane kesho rafiki tutajifunza zaidi kuhusu changamoto ya karne hii ya 21 na yale tunayopsawa kuchukua, hili tuendane na mabadiliko yanayotokea kwa kasi kubwa.
Makala hii imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio, ushauri nasaha na uandishi.
Maureen Kemei
Blog
Kufikirichanya.wordpress.com
Asante Uwazi utatusadia tusiwe bendera kufuata upepo
Kweli ili tuwe na msimamo wa kuwa focus na jambo moja.