30/100.Changamoto kubwa ya karne ya 21 na jinsi ya kuzivuka.

Karibu katika uendelezo wa kujifunza kutoka kitabu 21 lessons for the 21st century, ambacho kimeandikwa na Mwana historia Yuval Noah Harari.

Kimeelezea kwa kina sana changamoto tunazopitia kwenye karne hii na hatua tunazopaswa kuchukua ili kuzivuka.

MOJA;CHANGAMOTO YA KITEKNOLOJIA.

Katika hiki kilaelezea changamoto zote za kiteknolojia zinaanzia kwenye mambo mawili.

Moja ni ukuaji wa teknolojia wa habari INFOTECH ambayo sasa hivi taarifa za wengi zimekusanywa na makampuni makubwa ya kiteknolojia na hivyo kuweza kutushawishi kuchukua hatua fulani.

Mifumo ya kiteknolojia imeweza kukua sana kiasi cha kuweza kumjua mtu kuliko anavyojijua mwenyewe. Kama umekuwa unatumia Google au Facebook, utagundua mitandao inajua tabia zako kuliko wewe, hivyo inakuletea aina ya vitu unavyopendelea kufuatilia. Hii ni changamoto kubwa kama watu hatutakuwa na udhibiti wa taarifa zetu.

Mbili ni ukuaji wa teknolojia ya kibaolojia BIOTECH ambao kwa Sasa taarifa za ufanyaji wa kazi wa mwili wa binadamu zimeshakusanywa sana.

Kwa Sasa tuna uelewa mkubwa sana wa jinsi miili yetu inafanya kazi, jinsi ubongo unayofanya kazi na hata jinsi hisia mbalimbali zinavyoibuliwa kwenye mwili, kupitia kemikali mbalimbali ambazo mwili unazalisha.

Changamoto kubwa Sana itakuja pale teknolojia hizi mbili zitakapoungana, yaani INFOTECH na BIOTECH, kwa mfano kunaweza kuwepo na kadi ambayo inawekwa kwenye mwili wa binadamu, ambayo inasoma taarifa za mwili na kuzituma kwenye mfumo wa kompyuta kisha kompyuta kufanya maamuzi kwa ajili ya mtu huyo.

Mfano unapokuwa na huzuni, taarifa zinatumwa kwenye kompyuta kwamba una huzuni na hapo kompyuta inakuchagulia wimbo mzuri wa kusikiliza.

Kadhalika mgonjwa yatakuwa rahisi kugundulika kabla dalili hazijaanza kuonekana. Magonjwa mengi huanza kwa mabadiliko madogo madogo kwenye mwili ambayo hayana dalili za nje. Uwepo kwa mfumo unaokagua mwili utatoa taarifa haraka kuhusu mabadiliko hayo hivyo kuzuia ugonjwa kabla haujaanza. Magonjwa kama saratani yataweza kuzuilika mapema.

Mfumo kama huo unaonekana ni mzuri sana, lakini una hatari moja kubwa, taarifa za jinsi mwili wako unavyoendeshwa zikifika kwenye mikono ambayo siyo salama, unageuka kuwa mtumwa.

Pata picha taifa linaloendeshwa na Rais dikteta halafu ana nguvu ya kuwa na taarifa za wananchi wake wote, anaweza kuwafanya wajisikie vile watakavyo na hata wamtukuze na kumwona yeye ndiye mkombozi wao.

Kadhalika taarifa hizo zikifika kwenye mikono ya makampuni makubwa, yatazitumia kuhakikisha unakuwa mteja wao na kununua chochote wanachouza.

Hivyo pamoja na maendeleo haya makubwa yanayoweza kutokea kwenye sekta hizi,tunapaswa kuwa na udhibiti mkubwa wa taarifa zetu ili zisitumike kutufanya watumwa au wateja wa watu wengine.

Makala hii imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio, ushauri nasaha na uandishi.

Maureen Kemei
Blog
Kufikirichanya.wordpress.com

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

1 comment

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *