35/100.Utakapokua huenda usiwe na kazi.

Karibu sana tujifunze zaidi kutoka kitabu cha 21 lessons for the 21st century kimeandikwa na Mwana historia Yuval Noah Harari.

Zama zilizopita mtu alikuwa anapata kazi moja na kudumu nayo maisha yake yote. Hii ni kwa sababu mabadiliko yalikuwa yanatokea kwa kazi ndogo sana hivyo wengi waliweza kudumu na kazi moja maisha yao yote. Na msukumo mkubwa ukawa kwenye kusoma na kuwa na taaluma ambayo itakuwezesha kuwa na Kazi ya maisha.

Lakini katika karne hii ya 21, mabadiliko yanatokea kwa kasi kubwa mno,kazi nyingi zinapotea kila siku. Mifumo mipya ya teknolojia ya habari inaondoa uhitaji wa watu wengi kwenye kazi. Hivyo wazo la kuwa na Kazi ya maisha halipo tena. Maroboti yanaonekana kuchukua kila aina ya kazi ambazo zinafanywa na watu.

Njia pekee ya kukabiliana na hili ni kuwa tayari kubadilika kila wakati, kutokuishi na kufanya kazi kwa mazoea. Badala yake kujua mabadiliko yanaelekea wapi na kisha kuwa mbele ya mabadiliko hayo.

Angalia kama kazi au biashara unayofanya sasa inaathiriwa na mabadiliko yanayoendelea kwenye teknolojia ya habari na baiolojia, kisha chukua hatua mapema.

Mfano mzuri ni kwenye biashara ya taksi, wapo watu ambao wamekuwa kwenye biashara hii kwa muda mrefu, ikaja huduma au uba ambayo inamwezesha kila mtu kutoa huduma ya usafiri wa teksi, hii ikaathiri sana wale waliotegemea hii kama biashara yao kuu.

Sasa ambacho kitaleta athari kubwa zaidi ni pale magari yanayojiendesha yenyewe yatakapokuwa yanatoa huduma za teksi, hakutahitajika kabisa uwepo wa dereva. Kwa taarifa yako, tayari yapo magari yanayojiendesha yenyewe.

Huu ni upande mmoja tu wa kazi ya udereva lakini kila kazi inaathiriwa na mabadiliko makubwa yanayotokea. Mfano mpaka operesheni kwenye miili ya binadamu kubwa zinaweza kufanya na maroboti na umakini mkubwa kuliko zinavyofanywa na madaktari wanadamu.

Tunapata funzo leo kwamba tusing’ang’ane na kazi au biashara tunayofanya sasa, mambo yanabadilika kwa kasi, hivyo inabidi nasi tubadilike pia.

Imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio, ushauri nasaha na uandishi.

Maureen Kemei

Blog :kufikirichanya.wordpress.com

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *