36/100. Kufuatiliwa kwa ukaribu kuliko tunavyofikiri.

Karibu, tunazidi kujifunza changamoto zinazotukabili zama hizi, ikiwa leo tunaangazia, changamoto ya kufuatiliwa na wanaomiliki taarifa nyingi za watu. Kutoka kitabu cha 21 lessons for the 21st century kimeandikwa na Mwana historia Yuval Noah Harari.

Mwandishi anatusimulia kuwa kipindi cha nyuma wakati wa ukoloni, mataifa makubwa yalikuwa yanapigania kushika ardhi kwenye nchi nyingi. Hili lilizalisha ukoloni.

Anatujuza kuwa kwenye karne hii ya 21, Kuna aina mpya ya harakati kwa mataifa makubwa na hata kampuni kubwa. Makampuni haya yanapigania kupata taarifa za watu, kadiri wanavyokuwa na taarifa nyingi kuhusu mtu na kwa watu wengi, ndivyo inavyoweza kutumia taarifa hizi kusukuma watu kuchukua hatua fulani.

Makampuni makubwa kama google, facebook, Amazon, alibaba, Coca-Cola na mengineyo yapo kwenye harakati kubwa za kukusanya taarifa nyingi za watu. Kwa kadiri wanavyokuwa na taarifa nyingi kuhusu watu ndivyo wanavyowasukuma watumie bidhaa zao. Kadhalika kila taifa linakazana kupata taarifa zaidi za watu wake na hata watu wa mataifa mengine.

Hivyo yafaa tufahamu kwamba, tunafuatiliwa kwa karibu kuliko tunavyofikiri. Tunapoingia mtandaoni na kufanya yale yametupeleka uko. Na tukafanya mambo tofauti, tuijue kuwa kuna mifumo ya kompyuta inayofuatilia sana kuhusu sisi, tunapendelea nini na kadhalika.

Limeshaonekana kuwa, google na facebook zinatujua vizuri kuliko tunavyojijjua. Hali hii ni hatari sana kwa sababu itafika wakati tutaiamini mifumo hii ifanye maamuzi kwa ajili yetu na hapo tutakuwa tumechagua utumwa mbaya sana.

Sasa hivi karibu kila mtu anafanya maamuz kwa kutumia google, kama Kuna kitu unataka kujua, unauliza google. Kama Kuna mahali unataka kwenda lakini hupajui, ukiuliza google unapewa mpaka ramani ya kufika.

Kile tunachotoka nacho leo hii ni kuwa, twapaswa kuwa makini na taarifa tunazotoa kwa mifumo hii. Tunapaswa kuweka nguvu kubwa kwenye kujiendeleza sisi wanadamu, kukuza ufahamu wetu ili tusiishie kuwa na mifumo yenye uwezo mkubwa na wanadamu tunabaki na uwezo mdogo.

Kwani tukifikia hatua hii, tutakuwa tumekubali kuwa watumwa kwa vitu tulivyotengeneza sisi wenyewe.

Imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio, ushauri nasaha na uandishi.

Maureen Kemei

Blog ;kufikirichanya.wordpress.com

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *