38/100. Umuhimu wa jumuiya.

Ni katika harakati ya kujifunza zaidi kutoka kitabu cha 21 lessons for the 21st century ambacho kimeandikwa na Mwana historia Yuval Noah Harari.

Yale nimejifunza ni kwamba;

Sisi binadamu ni viumbe wa kijamii, tumezoea kuwa sehemu ya jamii kubwa. Kupona kwetu kama binadamu ni kwa sababu tuliishi kama jamii tangu enzi na enzi. Jamii ilikuwa msaada kwa wote, wale wenye nguvu na uwezo na wasiokuwa na nguvu na uwezo.

Katika karne ya 21 tunakabiliwa na changamoto kubwa ya kuvunjika kwa jumuiya nyingi, kuanzia za watu binafsi mpaka za mataifa au kitaifa. Tumeona baadhi ya mataifa kutaka kuvunjika yaliyokuwa yameungana na wengine kuachana. Baadhi ya mataifa yanataka kugawanyika.

Na katika hali binafsi hali ndiyo mbaya zaidi, ile nafasi ya watu kukutana ana kwa ana kama jamii imepungua sana. Sasa hivi watu wamekuwa wanakutana zaidi mtandaoni. Na hata wanaopata nafasi ya kuwa pamoja. Bado muda mwingi wanatumia kwenye mtandao wa kijamii, badala ya kutumia kwa mazungumzo ya pamoja.

Tunajifunza leo kuwa, tunapaswa kurejea kwenye misingi ya jumuiya, kwa kuimarisha ushirikiano wetu na wengine, hasa wa ana kwa ana. Kwa sababu utegemezi wetu kwenye teknolojia na mtandao wa kijamii umeleta hali ya kutengwa ndani yetu.

Tafiti nyingi kwa Sasa zinaonesha kiwango cha msongo na sonona kinaongezeka kwa wengi kwa kukosa nafasi ya kuwa ana kwa ana na wengine na kutegemea zaidi mtandao ya kijamii.

Tukutane tena kesho ili tufahamu changamoto zingine zinazotukabili zama hizi na namna ya kuzitatua au kuepukana nazo.

Imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio na ushauri wa maisha.

Maureen Kemei

Blog :kufikirichanya.wordpress.com

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *