39/100. Ustaarabu moja tu duniani.

Karibu, tunaendelea kufahamu changamoto za karne ya 21. Kutoka kitabu cha 21 lessons for the 21st century kimeandikwa na Mwana historia Yuval Noah Harari.

Dunia imepitia vipindi tofauti ambapo kila jamii ilikuwa na ustaarabu wake na namna ya kufanya mambo yake. Pia ndani kumekuwa  na mgawanyiko wa watu kulingana na dini au makabila yao. Hivyo ndani ya jamii moja bado kulikuwa na ustaarabu wa aina tofaut tofauti.

Lakini karne 21 mambo yamebadilika sana, kuna ustaarabu mmoja tu duniani, na jamii zote zinaishi kwa ustaarabu huo. Na hili limerahisisha mwingiliano baina ya jamii tofauti.

Ukichukulia mfano wa mchezo ya Olympic, ambayo inahusisha nchi zote duniani kinachowezesha michezo hii kuwezekana ni kuwepo kwa ustaarabu ambao unakubalika na kila nchi.

Ukiangalia pia kila nchi ina bendera yake, kila nchi ina wimbo wake wa taifa, kila nchi ina sarafu yake, ambayo inaweza kubadilishwa na sarafu ya nchi nyingine.

Hali hii ya kuwepo kwa ustaarabu mmoja duniani inapelekea pia matatizo yanayotokea kwenye jamii moja kuathiri  jamii nyingine.

Hivyo leo tunajifunza kuwa tunapaswa kufikiri namna ambavyo kila tunachokifanya kinavyoathiri wengine pia na siyo kujiangalia sisi wenyewe.

Imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio, ushauri nasaha na uandishi.

Maureen Kemei

Blog:kufikirichanya.wordpress.com

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *