Karibu, katika kujifunza kwetu kutoka kitabu cha 21 lessons for the 21st century ambacho kimeandikwa na Mwana historia Yuval Noah Harari.
Tumejifunza na kufahamu baadhi ya changamoto tunazokabiliana nazo katika zama hizi. Leo tunajifunza kuhusu uwepo katika mataifa.
Kwa kipindi kirefu dini zimekuwa na nguvu kubwa Sana kwenye jamii. Katika zama zilizopita dini na serikali zilikuwa kitu kimoja, viongozi wa dini ndiyo waliokuwa wakileta utatuzi na suluhisho la changamoto mbalimbali ambazo watu walikuwa wanapitia. Kama mvua hazikunyesha basi viongozi wa dini walifanya ibada au kutoa kafara na miungu ikajibu kwa kunyesha mvua.
Lakini katika karne ya 21 dini zimepoteza nguvu hiyo ya kutatua changamoto kubwa za kijamii. Lakini bado dini zimebaki na nguvu kubwa ya kuweza kuwaleta watu Pamoja. Watu wana imani kali kwenye dini na wengi wapo tayari kufanya chochote kwa jina la dini zao.
Watu hufanya hata uhalifu kwa kwa kisingizio kutetea dini zao. Kwa sasa mataifa yanayotaka kujitenga yanatumia nguvu ya dini katika kuwaleta watu pamoja. Hivyo dini zinakuwa chombo cha mataifa kuimarisha nguvu zao
Katika karne hii lazima tuelewe kwamba matatizo makubwa tunayokutana nayo hayawezi kupata majibu kwa kutegemea dini pekee. Lazima tujue kwamba kujitenga kwa mataifa kwa mwavuli wa dini kutazidi kutengeneza matatizo makubwa duniani.
Imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio, ushauri nasaha na uandishi.
Maureen Kemei.
Blog kufikirichanya.wordpress.com.