52/100. Maisha siyo hadithi.

Karibu, katika kujifunza zaidi kutoka kitabu cha 21 lessons for the 21st century ambacho kimeandikwa na Mwana historia Yuval Noah Harari.

Swali kubwa ambalo limekuwa linawasumbua watu tangu enzi na enzi ni nini maana ya maisha? Watu wamekuwa wakijiuliza swali hili na mengine kama mimi ni nani? Niko hapa duniani kufanya nini?

Katika kila zama swali la maana ya maisha ufanye nini na maisha limekuwa linapata majibu mbalimbali. Na majibu yote yanakuwa yanaletwa kwa hadithi

Hadithi moja maarufu ambayo imekuwa msingi wa dini nyingi ni kwamba kila mtu amekuwa duniani akiwa na kusudi lake tayari, na mtu akilitambua kusudi hilo na kuliishi basi atakuwa na maisha bora.

Kama hatajua kusudi lake au akalijua na asiliishi, basi maisha yake yatakuwa hovyo sana, hata kama atakuwa na mali nyingi kiasi gani.

Lakini pia zipo hadithi kwamba maana ya maisha ni yale tunayokutana nayo kila siku, mkusanyiko wa kila tunachpitia ndiyo maana ya maisha.

Na hadithi nyingine maisha ni mahaba, kwamba mtu akipata anachopemda na kuweka maisha yake yote kwenye kitu hicho amepata maana ya maisha yake.

Hadithi nyingi za maana ya maisha hazijakamilika na hili ndilo zinawafanya watu wasiridhike na maisha licha ya kuishi hadithi hizo.

Ili hadithi ya maisha ikamilike na iendane na wewe inapaswa kukidhi vigezo viwili, moja ikuhusishe wewe kama mhusika  mkuu na pili iwe na maana ambayo ni kubwa kuliko wewe.

Hadithi nyingi tunazoishi kwenye maisha ni za uongo, ni kitu ambacho kimetengenezwa na watu, lakini tunaziamini na kuziishi kwa sababu kila mtu anafanya hivyo. Na wakati mwingine inabidi tuziamini kwa sababu tulishajitoa sana uko nyuma kwa sababu ya hadithi hizo.

Hatua za kuchukua ;

Njia pekee za kujijua wenyewe, njia pekee ya kujua maana ya maisha siyo kwa kuangalia hadithi tunazoishi, bali kwa kuangalia mateso na kuelewa maana yake.

Sehemu kubwa ya maisha yetu ni mateso, hivyo Kuyaelewa maisha tunapswa kuanza na kuyaelewa mateso. Maisha siyo hadithi kama tulivyozoeshwa, bali maana ya maisha ipo kwenye mateso tunayopitia.

Ahsante kwa kusoma nakala hii, imeandikwa na mwanafuzi wa mafanikio, ushauri nasaha na uandishi.

Maureen Kemei.

Blog:kufikirichanya.wordpress.com

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *