Karibu rafiki, leo tunajifunza mbinu bora za mafanikio kwenye unenaji, kutoka kitabu cha the art of public speaking kilichoandikwa na waandishi Dale Carnegie na J. Berg Esenwein.
Wametushirikisha maarifa ya kujijengea kujiamini na kuweza kuongea mbele ya wengine kwa kujiamini na kwa mafanikio makubwa.
Moja ; njia ya kuishinda hofu ni kufanya.
Njia pekee ya kuishinda hofu ni kufanya kile kitu ambacho unahofia kufanya. Hii ndiyo hatua ya kwanza kabisa unayopaswa kuchukua ili kujijengea kujiamini na kuondokana na hofu ya kuongea mbele ya wengine, kwa kuongea zaidi mbele ya wengine.
Lengo linapaswa kuwa kutafuta fursa zaidi za kuongea mbele ya wengine.
Rafiki, hofu huwa ni hali ya kifikra zaidi kuliko uhalisia. Huwa tunatengeneza hofu kwenye fikra zetu kwa kutengeneza picha ambazo haipo.
Lakini tunapofanya kitu matokeo huwa ni tofauti kabisa na picha tuliyokuwa tunajipa awali. Hivyo kwa matokeo tunayopata, hofu inapungua yenyewe.
Mara ya kwanza kufanya kitu chochote huwa tunakuwa na hofu kubwa, lakini kadiri tunavyoendelea kufanya, hofu hiyo inakosa nguvu na kupotea kabisa.
Kinachowafanya wengi kuwa na hofu ya kuongea mbele ya wengine ni kwa sababu hawachukui hatua za kutosha katika kuishinda hofu hiyo.
Hatua za kuchukua.
Kila unapokuwa mbele ya wengine, tafuta nafasi ya kuongea chochote. Anza na vikundi vidogo vidogo kisha nenda kwenye makundi makubwa zaidi.
Kadiri unavyorudia rudia kufanya kitu, ndivyo hofu inavyokosa nguvu na mtu kujiamini zaidi. Tafuta nafasi zaidi za kuongea mbele ya watu na utaweza kuishinda hofu hiyo.
Ahsante kwa kusoma nakala hii, imeandikwa na mwana mafanikio na mshauri wako.
Maureen Kemei.
Blog, kufikirichanya.wordpress.com
Maisha yangu, uchaguzi wangu.