Karibu, tunaendelea kujifunza kutoka kitabu cha the art of public speaking kilichoandikwa na Dale Carnegie na J. Berg Esenwein.
Maandalizi ni muhimu sana katika kuongea mbele ya wengine. Kama unakwenda kuongea mbele ya wengine huku ukiwa huna maandalizi sahihi, hofu itakujaa na utafanya vibaya.
Ni muhimu sana uwe na kitu cha kusema na uwe na maandalizi mazuri katika kusema kitu hicho. Lazima uwe unajua kwa kina kile ambacho unazungumzia, iwe ni kwa kujifunza au kwa uzoefu.
Lakini kujua pekee haitoshi lazima pia uwe umejiandaa jinsi ya kusema kile unachojua, kwa namba ambayo watu wataelewa na kukupokea. Hivyo lazima ujiandae kwa kujua kile unachokwenda kuzungumzia na pia kujua njia bora ya kukisema kwa wengine.
Unapokuwa unakijua kwa kina kile unachosema na kuwa na maandalizi mazuri ya jinsi ya kukiongea, unakuwa unajiamini zaidi na hilo linaondoa kabisa hofu unayokuwa nayo wakati wa kuongea mbele ya wengine.
Ukienda kuongea mbele ya wengine bila ya maandalizi, hofu itakutanda na utasahau hata kile kidogo ambacho ulikuwa nacho.
Wanenaji wenye mafanikio makubwa wamekuwa wanafanya maandalizi makubwa. Kwanza wanajifunza sana kuhusu somo wanalonenea, pili wanafanya mazoezi ya jinsi ya kunena.
Wengi wanachukua muda wa peke yao na kusimama mbele ya kioo na kuigiza jinsi wanavyokwenda kuongea mbele ya wengine. Wengi wanarecodi sauti zao is a kujisikia jinsi wanavyoongea na kuboresha zaidi.
Hatua ya kuchukua.
Ni muhimu sana uwe na maandalizi ya kutosha ili uweze kuishinda hofu ya kuongea mbele ya wengine na uweze kuongea kwa kujiamini.
Ahsante sana kwa kusoma nakala hii imeandikwa na mwandishi na mshauri wako.
Maureen Kemei
Bloh:kufikirichanya.wordpress.com