Tunaendelea kujifunza namna ya kuwa chanya wakati wote, tuliangalia kwamba kuwa chanya au hasi inaanzia kwenye fikra zetu.
Ili tufikirie chanya au tuwe chanya wakati wote, inabidi tubadili mfumo wote wa kifikra. Kutoka hasi kwenda chanya ili tupate nafasi ya kuona fursa badala ya matatizo.
Kitu kinachotuzuia wakati mwingine tusifanye jambo bora ni kuwa na mtazamo hasi, hasa kama kitu ni kipya wengi wanakuwa na mtazamo ya kufeli au kushindwa.
Ili tuweze kushinda hali hii ya kuona kushindwa lazima tukatae kabisa fikra hasi. Hata kama wazo hilo linaonekana kutisha au kuwa ngumu, kuwa na mtazamo chanya kunakusukuma kuchukua hatua ya ziada itakayokuletea ushindi.
Uzuri sisi binadamu tuna uwezo wa kufikiri na kuamua maisha yetu yanafaa kwenda aje. Unaweza kuamua kufikiri chanya na kuona fursa au kutawaliwa fikra hasi na kuona matatizo mengi.
Asante kwa kusoma nakali hii imeandikwa na ;
Maureen Kemei
Mwandishi na anayekujali sana.
Maisha mema, chaguzi wangu.