Hatua za kutengeneza maisha bora na yenye mafanikio.

Hatua ya kwanza ni taswira, unapaswa kutengeneza taswira ya maisha unayotaka kuwa nayo. Kwenye taswira hii ndiyo unajua kusudi la maisha yako, unaweka maono yako, unakuwa na sababu ya kwa nini unataka kufikia maono hayo na hatua za kuchukua. Ni lazima kwanza uone taswira cha unachotaka kabla hakijatokea kwa uhalisia.

Hatua ya pili ni utambuzi baada ya kupata picha ya wapi unakotaka kufika, kinachofuata ni kutambua njia unayopaswa kupita ili kufika kwenye maono yako. Anzia hapo ulipo Sasa, kwa hali uliyonayo sasa. Usisubiri mpaka kila kitu kiwe Sawa ndiyo uanze, kwa sababu hakuna wakati ambao kila kitu kitakuwa Sawa. Kuanza ni bora kuliko kusubiri.

Hatua ya tatu, maboresho unapoanza ukiwa hujawa tayari, utajifunza kadiri unavyokwenda. Hivyo utaona njia bora zaidi za kufika kule unakotaka kufika, na hapo unapaswa kufanya maboresho ili kufika unakokwenda. Kwa kila hatua unayochukua, jiulize unawezaje kuboresha zaidi. Maboresho madogo madogo yanyofanywa kila siku yanakuja kuzalisha matokeo makubwa na ya tofauti kabisa.

Hatua ya nne ni ubunifu, kupata matokeo ya tofauti na unayopata sasa ni lazima uchukue hatua tofaut na unazochukua sasa. Unahitaji kuwa mbunifu na ubunifu ni kufanya vitu kwa namna tofauti. Unaweza kufanya vitu kwa utofauti kwa kuanza na mtazamo Tofauti, kuangalia kitu kwa namna tofauti na kujaribu vitu vipya ambavyo hujawahi kufanya huko nyuma. Kwa kila unachofanya, jiulize ni kwa namna gani unaweza kufanya kwa utofauti na ukapata matokeo bora.

Hatua ya tano utekelezaji, mipango haiwezi kukuletea mafanikio, nia njema haitakutoa hapo ulipo sasa, ni mpaka pale utakapochukua hatua ya kutekeleza yale uliyopanga ndiyo utaweza kutoka hapo ulipo Sasa na kufika unakoelekea. Ni kuchukua hatua ndiko kutakakokubadili wewe kutoka hapo ulipo sasa na Kufikia maono yako makubwa. Wanaofanikiwa ni wale wanachukua hatua, wakati wale Wasiofikiria kuchukua hatua wakibaki pale walipo sasa.

Hatua ya sita ufahamu, kila siku Kuna ufahamu ambao tunaupata kupitia yale tunayofanya. Iwapo tunatambua au kutokutambua ufahamu huo kunaamuliwa na utayari wengi kutenga muda na kutafakari kwa kina kila hatua tunayopiga. Tunapotenga muda wa kutafakari, kukaa kimya, kusikiliza na kuangalia, tunajifunza vitu vingi ambavyo siyo rahisi kuviona kama tumetingwa na majukumu yetu ya kila siku. Ufahamu tunaoupata una mchango mkubwa kwenye mtazamo wetu, unatutengeneza jinsi tunavyofikiri leo kuhusu tunachotaka kufikia kesho.

Hatua ya sapa ni kujihami, siyo kila kitu kitaenda kama tunavyopanga. Kuna wakati tunapata matokeo hasi na kukutana na watu hasi amabo watakukatisha tamaa kuhusu malengo unayofanyia kazi, kwa kukuambia haiwezekani au huwezi. Watu hawa wanaweza kuwa marafiki, ndugu wa karibu, familia au hata wale unaofanya nao kazi. Jihami na watu hao hasi kama unataka kufanikiwa, kwa sababu uwepo wao kwenye maisha yako utakuwa kikwazo kwako kufanikiwa zaidi. Na hapa haimaanishi kuwatenga, bali kuhakikisha hawaleti ushawishi wao hasi kwenye ndoto zako, kwa kuchagua kutokuwashirikisha ndoto hizo.

Njia rahisi ya kuwajua watu hasi unaopaswa kujihami nao ni kuangalia watu hao wanakuwa na majibu gani unapowaeleza kuhusu mafanikio makubwa. Kama ni watu wanaoamini haiwezekani, basi waweke kwenye kundi la watu hasi na chukua hatua sahihi kwao.

Hatua ya nane ni uwekezaji, kufikia yote unayotaka kufikia na ambayo yapo ndani ya uwezo wako unapaswa kuwekeza muda, nguvu, juhudi, moyo na fedha. Kila mtu anataka kufanikiwa na kupata matokeo bora kwake na kwa familia yake, kila mtu anataka kilicho bora. Lakini kipimo sahihi cha nani anachotaka, ni utayari wa uwekezaji amabo mtu anao. Unapowekeza vitu hivyo vitano, ndipo unaiambia dunia umejitoa kweli kufanikiwa na hakuna chochote kitakachokuzuia.

Unawekeza muda, kwa kutoa muda wako kufanyia kazi malengo yako. Unawekeza nguvu kwa kuweka juhudi katika kuyafikia malengo yako. Unawekeza juhudi kwa kwenda hatua ya ziada kwa Kil unachofanya. Unawekeza moyo kwa kuwa na hisia chanya juu yako binafsi na kile unachofanya. Unawekeza fedha kwa kununua maarifa na ujuzi unaopaswa kuwa nayo ili kufanikiwa.

Unaleta pamoja vitu hivyo vitano kwenye kile unachokifanya, nguvu kubwa usiyoweza kuielezea kinakuwa kwako na kukuwezesha kufikia malengo ambayo umejiwekea.

Nakala hii imenakiliwa na mwandish na mshauri.

Maureen Kemei.

Maisha yangu, uchaguzi wangu.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *