Jinsi ya kujizuia kuingia kwenye hasira.

Je kuna uzuri wowote kwenye hasira? Je Kuna uzuri wowote tunayoweza kupata kwa kuwa na hasira? Haya ni maswali ambayo Seneca alijiuliza na kujipa majibu. Kutoka kitabu chake cha( Anger, book 2.)

Karibu tujifunze nasi ili tujue namna ya kujizuia wakati tunapatwa na hasira.

Kinachoibua hasira ndani yetu siyo kile ambacho kimetokea, bali jinsi tunavyofikiria kuhusu kilichotokea. Tunapatwa na hasira pale tunapoamini kwamba tumekosewa na wengine na hivyo kuwa na nia ya kulipa ule ubaya ambao tumefanyiwa.

Hasira ni zao la kutotumia vizuri fikra zetu, pale hasira zinapoibuliwa ndani yetu na sisi kulipuka kwa hisia hatutumii vizuri fikra zetu. Hivyo kama mtu utasimamia kutumia fikra zako, hasira haiwezi kukutawala.

Wengi wamekuwa wanajiambia kwamba hawawezi kuacha kuwa na hasira kwa sababu wakosaji ni wengi sana sasa kama utatumia hicho kama kigezo cha hasira, basi hutaacha kuwa na hasira, kwa sababu hakuna siku itakayoanza mpaka iishe asitokee mtu wa kukukosea. Wapo wanaokosea kwa makusudi na wapo wanaokosea kwa kutokujua.

Kwa namna yoyote ile Seneca anatushauri usimkasirikie mtu yeyote anayekukosea. Asante kwa kusoma nakali hii, imeandikwa na mwandishi na mshauri.

Maureen Kemei.

Blog, kufikirichanya.wordpress.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

1 comment

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *