Rafiki tunaendeleza mafunzo yetu kutoka kitabu cha anger book 2,kilichoandiwa na Mwana falsafa Seneca.
Kila unapotaka kupata hasira juu ya makosa ya wengine, jiulize je unaweza kuwa na hasira kwa mtoto mchanga ambaye haachi kulia? Unapoanza kuwachukulia watu wengine na makosa yao kwa mtazamo huo, ndipo unaona kuwa hasira haina maana yoyote.
Ili kuondokana na kukasirishwa na wengine, unapaswa kuwa mtu wa kumsamehe kila mtu, binadamu wanahitaji huruma na msamaha kwa sababu kila mmoja wetu ni mkosaji kwa namna moja au nyingine. Unaweza kuwakasirikia wengine waliofanya makosa fulani, lakini kumbuka ata wewe Kuna makosa ulifanya, huenda tu hayachulikani.
Mtu mwenye hekima huwa hakasirishwi na wengine, kwa sababu anajua watu hawataacha kukosea. Na hivyo anapoamka anajua kabisa katika siku yake atakutana na watu wakosefu, watu wavivu, watu wenye hila na tamaa. Na yeye anajua atakabiliana na tabia hizo kama daktari anavyokabiliana na ugonjwa kwenye mwili wa mtu.
Daktari hawi na hasira kwa mtu kwa sababu anaumwa, bali anachukua hatua kutibu ugonjwa wake. Hivyo ndivyo inavyopaswa kuwa kwa wakosaji, tusiwakasirikie, badala yake tuwasaidie pale wanapokwama.
Asante kwa kusoma nakali hii imeandikwa na mwandishi na mshauri.
Maureen Kemei.
Blog, kufikirichanya.wordpress.com.