Kila mtu ana ndoto kubwa kwenye maisha yake, tukiwa wachanga huwa tunaulizwa unataka kuwa nani, majibu huwa ya haraka sana labda daktari, piloti, raisi na mengineyo.
Lakini unapofikia kiwango cha chuo ukiulizwa unataka kuwa nani wengi huwa tumesahau au tunakwepa kusema ndoto hiyo kubwa iliyo ndani yetu. Tunaanza kuwa wa kawaida kabisa na kufuata jamii wanasema nini juu yetu.
Kitu kubaya sasa ni pale unapokuwa na msukumo mkubwa wa kufanya jambo, unaanza kuhairisha polepole ukijiambia hujawa tayari, au bado muda unayo.
Tunajua jinsi ambavyo hatuna uhakika wa muda wetu hapa duniani. Tunajua jinsi wengi wanavyokuja kujuta maisha yao yanapofika ukingoni. Usiwe mtu wa aina hiyo, usiwe mtu wa kuahirisha ndoto zako.
Badala yake zitekeleze ndoto zako kama unavyoziona kwenye akili yako. Hata kama wengine hawatakuelewa, fanya kile unachojua ni sahihi, mana kama ni majuto wewe ndiye utayeyapata.
Muda tulionao ndiyo huu, hakuna wakati utakuwa tayari zaidi ya ulivyo sasa. Anza kuziishi ndoto zako sasa kwa pale ulipo na kwa kile ulichonacho sasa. Hiyo ndiyo njia ya kuwa na maisha kamilifu.
Asante kwa kusoma nakali hii naamini unaishi ndoto zako, ama kama ulikuwa umesahau unaanza kuishi sasa. Imeandikwa na mwandishi na mshauri.
Maureen Kemei.
Email ;kemeimaureen7@gmail.com.