Katika zama hizi ni vigumu sana kwa watu wengi kuweka umakini wao kwenye kitu kimoja. Hasa kwenye kusoma au kuandika au kutafakari jambo moja kwa muda fulani.
Wengi hudhani hawawezi kudhibiti fikra na akili zao, lakini ni jambo linalowezekana kabisa. Nguvu ya udhibiti wa fikra ipo kwa kila mmoja wetu, tunahitaji kuiendeleza kwa kukadiria kabisa kujitafutia utulivu na kujaribu kurudisha fikra kwenye jambo moja.
Kama vile tunavyoweka juhudi kwenye kutunza miili yetu, kuanzia kulisha, kuisafisha na kuvalisha. Hivyo ndivyo inavyotupasa kuweka juhudi kwenye utunzaji wa fikra zetu, kwa kudhibiti akili zetu kutokuzurura kwenye mambo mengi.
Unafanya hili kwa kuchagua kuweka mawazo yako kwenye vitu ambavyo vina manufaa zaidi. Hapo unakuwa umeidhibiti akili yako, lakini pia unakuwa umefikiria na kutafakari kitu ambacho ni muhimu kwenye maisha yako.
Tumejifunza leo kuwa kwa namna yoyote ile usiache tu akili yako izurure hovyo, badala yake idhibiti kwa kuweka mawazo yako kwenye kitu kimoja kwa muda mrefu. Na hapo utaweza kwa muda fulani kuona matokeo mazuri, lakini akili na fikra zikizurura kila mara hakuna jambo la maana unaloweza kuitimiza.
Asante kwa kusoma nakali hii imeandikwa na mwandishi na mshauri.
Maureen Kemei.
Email ;kemeimaureen7@gmail.com
Bloh;kufikirichanya.wordpress.com
Hii ni kweli kabisa asante