Umuhimu wa kuthamini kile ambacho unacho.

Binadamu kwa asili tunatamani vitu ambavyo hatuna. Tunatamani vile ambavyo wengine wanavyo na kusahau hata vile ambavyo tunavyo.

Usiweke akili yako kwenye vitu ambavyo huvimiliki na siyo vyako, lakini ni vyema kuhesabu baraka zako kwenye vitu ambavyo unavyo.

Uhuru kamili ni kutumia kile ambacho unacho. Kile ambacho siyo yako ni utumwa, maana utakaa kuwa na wasiwasi kama mwenyewe ataulisia.

Kitu kingine ni kutumia kile ambacho unacho vizuri maana Kuna siku utavikosa. Hiyo siku ndio utaumia sana kwa kupoteza kile ambacho ulichonacho.

Kuna vitu vingi tunavimiliki na hatuvithamini, tukianzia kwenye mahusiano watu wengi huchukua mwenzake kama wa kawaida tu, lakini siku ambayo hayuko ndio utagundua ni wa maana akiwa karibu nawe.

Vitu kama fedha siku ambayo huna ndio unakumbuka unahitaji fedha ili kununua mahitaji muhimu. Watu wa karibu kama wazazi wengi hawakumbuki kuwatunza wazazi wakiwa hai, siku ambayo hawapo wanaanza kujilaumu mbona hawakuwatunza wakiwa hai.

Hatua ya kuchukua leo ni kuweka nguvu kwenye kile ambacho unacho sasa. Usipoteze nguvu kwenye kile ambacho huvimiliki.

Hivyo basi, vyote tunavyovimiliki tumeazimwa na asili kwa muda tu. Kazi yetu ni kuthamini na kuvitumia vizuri hata siku ukija kuondoka hutajutia. Ubaya unakuja pale ulikuwa na kitu alafu hukitumii wala hukithamini.

Imeandikwa na mwandishi na mshauri.

Maureen Kemei.

Blog, kufikirichanya.wordpress.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *