Karibu rafiki, tunajifunza leo kuhusu maadui makubwa mawili ambayo wanatukabili kwenye maisha yetu ya kila siku. Ukiacha hadaa ya sinema za maigizo ambazo zinaonyesha adui mkuu ni kitu cha nje, Kuna maadui halisi ambao unapaswa kuwakabili katika kujenga ushujaaa wako.
Katika kitabu cha the dedicated by Pete Davis, anatushirikisha kuwa kuna maadui wa ndani, ambapo wapo ndani yako, tukiachana na ya sinema.
Anasema kuwa adui wa kwanza ni hofu, ziko ndani yako, kuna hofu kuu tatu ambazo ni hofu ya kujutia, hofu ya mahusiano na hofu ya kupitwa.
Hofu hizo zinakuzuia usijitoe kwenye kitu kimoja kwa muda mrefu na kuweza kujenga ushujaaa unaohitajika kuleta mabadiliko.
Adui wa pili ni uchoshi, kwenye sinema za maigizo kila wakati Kuna tukio jipya la kusisimua, ndiyo maana tunaweza kuangalia sinema hizo kwa muda mrefu.
Lakini kwenye uhalisia, matukio ya kusisimua ni machache sana. Kwa muda mrefu unahitajika kufanya mambo ya kawaida na yanayojirudia rudia kwa muda mrefu.
Hii inaleta hali ya uchoshi ambayo ni rahisi sana kumkatisha mtu tamaa, hasa pale matokeo yanapokuwa hayaonekani kwa haraka. Ukichangia na wingi wa machaguo na usumbufu unaomzunguka mtu, ni rahisi sana kuacha kile anachofanya pale anapokutana na uchoshi.
Mashujaa walioweza kufanya makubwa ambao mpaka sasa tunawakumbuka, waliweza kuwavuka maadui hao makubwa wawili na kujitoa kwenye kile walichochagua.
Waliondokana na hofu za ndani na kuchagua kitu sahihi watakachopambana nacho kwa muda mrefu. Waliweza kuvuka uchoshi waliokutana nao kwa Kuendelea na mchakato bila kuruhusu usumbufu kuwaingilia.
Chukua hatua leo, kwa kuamua kufanya kitu kwa kuirudia rudia bila kuacha kwa muda mrefu, zinajikusanya na kuleta matokeo makubwa baadae. Sharti hatua hizo ziwe endelevu bila ya ukomo.
Wengi huja kushangaa wanapoona matokeo na kuuliza imewezekanaje? Ni hatua ndogo ndogo ndizo zinachangia matokeo makubwa, uwe na siku njema.
Akujaliye sana,
Maureen Kemei.
Blog, kufikirichanya.wordpress.com
Email, kemeimaureen7@gmail.com.