Kutumia kila fursa kuyafurahia maisha.

Katika maisha Kuna mambo mengi sana ambayo yanatufanya tukasirike na kukata tamaa. Lakini haifai tuliruhusu hilo litokee, lazima tutumie kila fursa tunayopewa kufurahia Maisha.

Maana maisha enyewe ni mafupi mno, hivyo kukasirishwa na vikwazo mbalimbali hayatasadia kusuluhisha au kurahisisha lolote kwenye maisha.

Kwenye kitabu cha everyday manifesto, Robin anatushirikisha kisa kilichotokea akiwa Dubai kutoa mafunzo kwa wagurunzi wa makampuni.

Akiwa kwenye lifti alikutana na mtu aliyevaa kofia aliyoipenda sana. Ndani yake akasukumwa Kusifia mtu huyo, lakini akasita kwa kuona huenda mtu huyo asipokee hilo vizuri.

Lakini akajiambia ni bora tu aseme, maana hatari kubwa kwenye maisha ni kutokuchukua hatua yoyote, akamwambia ameipenda sana kofia lake,mtu yule alitabasamu, kisha akavua kofia na kumpa kama zawadi.

Robin Alishangazwa na hilo, hakutegemea, alisukumwa tena kuikataa zawadi hiyo, ila akaikubali. Walipotoka kwenye lifti alienda kwenye gari na kuchukua kitabu chake na kumpa tu yule mtu, ambapo naye alikifurahia sana.

Kisa hiki kinatufunza kutumia kila fursa kuyafurahia maisha, kuwa mwema na kufanya yaliyo sahihi. Ni kwa hatua ndogo ndogo ndiyo mtu unajenga mafanikio yako makubwa.

Chukua hatua, furahia kila fursa kwenye kila siku yako,vijana wa sasa wanaita chagamkia kila fursa na hapo ndipo utashinda vikwazo na kukasirishwa hovyo na mambo madogo yanayotokea.

Akujaliaye sana, Maureen Kemei.

Blog, kufikirichanya.wordpress.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *