Habari na karibu.
Mabadiliko binafsi yanahitaji nafasi hili kutokea. Yaani kujaribu kuleta kitu kipya kwenye maisha yako. Unahitaji sehemu ya kukiweka vitu hivi vipya, hivyo inakubidi uondoe vya zamani.
Tumezoea kuambiwa tuache vitu vibaya na visivyokuwa na manufaa kwetu. Lakini Kuna upande mwingine wa hilo, kuacha vitu vizuri na tunavyovipenda ili kutengeneza nafasi ya vitu bora zaidi.
Ni lazima uache chochote kwenye maisha yako, hata kama unakipenda kiasi gani. Kama kuna kitu unajiambia huwezi kukiacha basi jua hicho kina nguvu ya kukutawala na umeshakuwa na uraibu nayo.
Hili tuwe huru na tuhakikishe tunafanya makubwa, lazima tuhakikishe hatupotezi uhuru wa kuamua kuacha chochote. Hivyo, kufanyia kazi uhuru huo mara kwa mara.
Chukua hatua, kila unapokiona unakitegemea sana kitu na kujiambia huwezi ukakiacha au kukikosa, hapo papo amua kabisa akiache. Hilo litakufundisha kwamba uwezo wako ni mkubwa kuliko chochote kile.
Asante rafika uwe na siku na #sambazauchanya #fikrachanya.
Akujaliaye sana, Maureen Kemei.
Blog, kufikirichanya.wordpress.com
Email, kemeimaureen7@gmail.com