Hofu siyo adui

Kila mtu huwa anahofia, kila anayefanya kazi kwa mara ya kwanza anakuwa na hofu kubwa. Hata wale wanaoonekana ni majasiri, ndani yao huwa wanakuwa na hofu kubwa. Lakini huwa wanaweza kuzishinda hofu hizo kwa sababu ya mtazamo wanaokuwa nao.

Mabadiliko makubwa ya kimtazamo inayoshauriwa kuyafanya ili kuyashinda hofu ni kuyajua kwamba hofu siyo adui. Hofu siyo kitu ambacho kinalenga kukuangusha na kukushinda. Hofu ni tahadhari ambayo akili yako inakupa, kwa lengo zuri la kuhakikisha unakuwa hai na salama.

Hofu ndiyo imekiwezesha kizazi hadi kizazi kuwa hai mpaka leo. Ni kwa sababu hofu inaleta tahadhari na mtu anapochukua tahadhari hiyo anakuwa salama. Hivyo tunapswa kuchukulia hofu siyo kama kikwazo cha kutufanya tusimame, bali kama tahadhari ya kwenda kwa umakini.

Hatuhitaji kuivunja kabisa hofu ndiyo tuweze kufanya makubwa. Tunachohitajika kufanya ni kuisikiliza, kuielewa na kuchukua hatua uku tukiwa na tahadhari. Hofu huwa inaonekana ina nguvu kwa sababu inagusa zaidi hisia zetu. Na pale kitu kinapogusa hisia, huwa tunakipa uzito zaidi.

Kuchukua hatua ndiyo njia pekee ya kuivuka hofu yoyote tunayokuwa nayo. Kama tulivyoona, hofu inatuingia kupitia fikra na hisia. Na kadiri unavyoitafakari hofu, ndivyo unazidi kuiba nguvu kubwa.

Njia pekee ya kuivuka hofu ni kuchukua hatua, kufanya kile unachohofia kufanya. Baada ya kuisikiliza na kuielewa hofu, unapaswa kuchukua hatua. Haipaswi uendelee tu kuitafakari, badala yake chukua tahadhari ambazo hofu inakupa kisha chukua hatua.

Unapochukua hatua na kupata matokeo mazuri, unazidi kujiamini na kupata hamasa ya kuchukua hatua zaidi. Pale hofu inapokuwa kali na ukashwishika uache kufanya. Usisikilize hofu, badala yake chukua hatua. Hata kama itakuwa hatua ndogo kiasi gani, Ina nguvu ya kuivuka hofu unayokuwa nayo.

Asante ni haya kwa leo, uwe na wakati mwema na #fikrachanya #sambazauchanya.

Akujaliye sana, Maureen Kemei.

Blog, kufikirichanya.wordpress.com

Email, kemeimaureen7@gmail.com

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *