Jinsi ya kutuliza hofu isiwe kikwazo kwako.

Karibu, changamoto kubwa kabisa kwenye hofu ni pale tunaposhindwa kuielewa kwa undani. Unapoiona hofu kwa nje inakuwa inatisha sana. Usipochambua kwa undani, hutaweza kupiga hatua, maana utaona ni kikwazo kikubwa.

Kwa kila hofu unayokuwa nayo, usiishie tu kuangalia kwa nje, bali ichimbe kwa undani, uweze kuielewa na kuchukua hatua sahihi. Hatua muhimu ya kuchukua ni kujiuliza kipi kibaya zaidi kinachoweza kutokea?

Kwa chochote unachohofia, usikubali tu hofu hiyo kwa juu juu. Badala yake chimba ndani, jiulize kipi kibaya zaidi kinachoweza kutokea kwenye hilo unalohofia? Jiulize kama kweli hofu hiyo itakutokea kama unavyohofia, ni mambo gani mabaya kabisa yanayoweza kutokea?

Orodhesha yote mabaya unayoona yanaweza kutokea kutokana na kile unachohofia. Kwa kila unaloorodhesha jiulize ni hatua zipi unazoweza kuchukua kulikabili kama kitatokea.

Kisha andika hatua zote unazokwenda kuchukua pale jambo baya kabisa linapotokea ili uweze kurudi kwenye mipango yako.

Kwa kufanya zoezi hili, unagundua wazi kwamba mambo mengi unayohofia hayawezi kutokea na hata kama yatatokea una njia ya kuweza kuyavuka na Kuendelea na mipango yako.

Kwa mfano unapowaza kuanzisha biashara hofu ni itashindwa. Kibaya zaidi kinachoweza kutokea ni biashara kufa na ukapoteza kila kitu. Kama hilo kitatokea unaweza kuanza upya, hata kwa kutafuta kazi au kibarua kwanza ili uweze kujijenga upya.

Chukua hatua , kwa kuamua kabisa kuchambua kile unachohofia kwa undani, unaona wazi kwamba unachohofia sana halipaswi kuwa kikwazo kwako.

Akujaliaye sana.

Mwandishi na mshauri.

Maureen Kemei.

Blog, kufikirichanya.wordpress.com.

Email, kemeimaureen7@gmail.com

#fikrachanya #sambazauchanya.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *