Ukweli kuhusu kushindwa

Wakati mwingi huwa nasikiliza wachungaji wa madhehebu mbalimbali wanapohubiri. Lakini kati ya wote Kuna menye nawasikiliza napata tumaini la kusonga mbele zaidi. Hata kama kwa wakati huo kuna jambo ambalo limenikwaza sana.

Mchungaji huyo huwa anapenda kusema kuwa “wakristo huwa hawashindwi au hawapati hasara, bali wanajifunza kupitia kushindwa kwao au hasara kwenye biashara ama kazi yoyote wanayofanya.”

Anasema kuwa Mungu huwaweka watu kwenye darasa kwanza wakikosa wanachotaka ndipo watakuwa wamejifunza njia isiyo sahihi ya kupata kile unachotaka.

Hivyo unachopaswa kufanya ni kujifunza njia iliyo sahihi ya kupata unachotaka. Unapojifunza kupitia unachokosea unajua ni njia zipi zisizo sahihi hili usizirudie.

Kushindwa ni pale tu unapokuwa umekata tamaa na unaporudia makosa yale yale. Lakini unapokuwa tayari kujifunza na kuboresha zaidi, hakuna kushindwa, badala yake Kuna kujifunza.

Kukosa unachokitaka haimaanishi kwamba huwezi kukipata, bali inamaanisha hujajua njia sahihi ya kukipata. Hivyo wajibu wako ni kujifunza njia iliyo sahihi na kuitumia.

Wewe mwenyewe ni shahidi, magumu mengi uliyopitia kwenye maisha yako na kuona kama umeshindwa, yamekuwa na mchango mkubwa kwako kupika hatua.

Chukua hatua, hakuna unachopitia kisiwe na manufaa kwako kama utakuwa tayari kujifunza na kuchukua hatua sahihi.

Akujaliaye, Maureen Kemei.

Blog, kufikirichanya.wordpress.com

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *