Jinsi ya kufikiria kila mtu ashinde.

Kwenye ushirikiano wetu na watu wengine, iwe ni kwenye kazi, biashara na hata maisha kwa ujumla, Kuna wakati tunajikuta kwenye majadiliano au kutokukubaliana.

Katia nyakati kama hizi ndipo mvutana mkubwa sana unapotokea na katika hali hii watu wenye ufanisi wanatofautiana sana watu ambao hawana ufanisi.

Watu wenye ufanisi wanafikiria kila mtu ashinde, yeye ashinde na wengine nao washinde. Lakini wasiokuwa na ufanisi hujifikiria wao wenyewe, washinde tu na wengine washindwe.

Katika hali hizi za kutokubaliana Kuna matokeo sita, moja wote mshinde, mbili, wewe ushindwe mwenzako ashinde, tatu wewe ushindwe mwenzako ashinde, nne wote mshindwe, tano wewe ushinde bila kujali mwingine anapata nini na sita melewane au hakuna makubaliano.

Stephen Covey kwenye kitabu chake cha “habits of highly effective people,” anatushirikisha namna tunaweza jenga hali ya majadiliano ambayo tunaweka mbele kila mmoja bila kujiona wenyewe.

Anatushirikisha kuwa ushindani wa moja kwa moja ambapo mtu mmoja anataka kushinda na mwingine ashindwe unaondoa ushirikiano na ubunifu. Kama eneno la kazi lina ushindani huu, labda ni zawadi kwa anayeshinda, inaua ushirikiano na hatimaye wote kuwa na uzalishaji mdogo. Watu wenye ufanisi mkubwa hawajiingizi kwenye mashindano.

Jamii zetu zimejengwa kwenye mfumo wa ushindani, kuanzia kwenye mfumo wa elimu ambapo anayepata alama A anaonekana mshindi na anayepata C anaonekana ameshindwa, kwenye michezo pia ni hivyo. Hali hizi zinawafanya watu wanafikiria ushindani kwenye kila jambo na hivyo  kuondoa ushirikiano na kupunguza ufanisi.

Kama wote hamshindi basi wote mnashindwa. Katika majadiliano yoyote ambapo Kuna mvutano, njia pekee ya wote kufaidika ni wote kushinda, kama wewe utashinda na mwenzako atashindwa basi wote mnakuwa mmeshindwa kwa sababu wakati mwingine utaikosa fursa kama hiyo.

Watu wenye ufanisi mkubwa mara zote wanaangalia ni jinsi gani kila mtu anaweza kunufaika na hili linawezesha kushirikiana na wengi na kufikia mafanikio makubwa.

Hatua ya kuchukua :kuanzia sasa kila unapojikuta kwenye hali ambayo inaleta ushindani, usitake kushinda wewe tu, bali angalia ni jinsi gani wengine nao wanaweza kunufaika. Kwa kujijengea tabia hii utaweza kushirikiana na wengi na utapata mchango makubwa kutoka kwa wengine.

Hii litakuongezea ufanisi na  kukuletea mafanikio. Si ustaarabu kukimbilia kushindana, mashindano yoyote mwisho wa siku yatakupoteza.

Akujaliaye sana

Maureen Kemei

Mshauri na Mwandishi.

Blog, kufikirichanya.wordpress.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *