Kwa nini ni muhimu kuwa na subira kwenye maisha.

Mambo mazuri kwenye maisha huwa hayataki haraka, hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye mafanikio, kama unataka mafanikio makubwa lazima uwe na subira.

Watu wengi hasa kwenye zama hizi tunashindwa kuwa na subira, hasa kwenye safari ya kutaka kufanikiwa. Kwa sababu wengi wetu tuna haraka ya kutaka kufanikiwa, hivyo kuweka muda wa kutosha ili kufikia mafanikio hayo ni jambo gumu kweli.

Kwa hivyo wengi tunataka njia ya mkato, lakini njia iyo ya mkato haileti mafanikio ya kudumu. Mtu yeyote anayejua kile anachotaka, na ambaye yuko tayari kuweka kazi kukipata, ni swala la muda tu, akiwa na subira ung’ang’anizi na uvumilivu, lazima atapata anachotaka.

Kitu ambacho tunapaswa kujua ni kuwa mambo yanatokea kwa wakati wake yenyewe, siyo kwa wakati unopanga wewe. Chochote unachotaka utakipata kwa wakati wake, lakini haitakuwa wakati uliopanga wewe.

Hivyo usione kama unachelewa kupata unachotaka na kukata tamaa, kuwa na subira, endelea na mchakato na wakati sahihi utakapofika, utapata unachotaka.

Ili uweze kuwa subira, acha kuhesabu na fanya sehemu yako. Wewe weka mkazo kwenye mchakato na siyo matokeo au muda ambao umeweka juhudi. Kadiri mchakato na muda unavyokwenda, ndivyo unajiweka kwenye nafasi nzuri ya kupata kile unachotaka.

Kila mtu anataka utajiri wa haraka na kwa njia ya mkato, lakini dunia huwa ina namna yake sahihi ya kukamilisha mambo, huwezi kuilazimisha bila ya kuleta madhara.

Hatua ya kuchukua, ni lazima uweke juhudi na muda ndiyo dunia ifikie hatua ya kukupa kile unachotaka. Na kama ambavyo tunajifunza kwamba hakuna mafanikio ya haraka, lazima tuweke kazi, tuwe na subira na tuweke muda wa kutosha, baadae bila pingamizi yoyote mafanikio utayapata.

Akujaliaye sana.

Mshauri na Mwandishi.

Maureen Kemei

Blog kufikirichanya.wordpress.com

Email, kemeimaureen7@gmail.com

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *