Tumekuwa tukisikiliza maneno haya kila wakati, “kaa chanya,” “usikubali kuwa na mtazamo hasi,” ” fikiria mawazo ya furaha.”
Misemo kama hii mara nyingi hutumiwa kututia moyo tunapohisi kuchanganyikiwa au tukiwa kwenye changamoto fulani.
Hata hivyo tunaweza kuwa tunasikia maneno haya na bado tunajisikia tupu kabisa au kuona kwamba hayatusaidii.
Lakini namna gani ikiwa ungeweza kutumia uwezo ulio ndani yako kufikiri vizuri hili kuboresha maisha yako. Kuamini kikweli uwezo ulio ndani yako juu ya hali njema yako?
Je, ikiwa utaruhusu uchanya utengeneze mawazo, hisia na tabia zako. Kubadilisha sauti za uchovu na kujipa imani ya kweli kwamba unaweza kupambana na mtazamo hasi ulio katika akili zako?
Kwa bahati nzuri, utafiti unaonyesha kupunguza mazungumzo hasi ya kibinafsi na kuchukua mawazo chanya zaidi Kuna faida nyingi za kiafya na kisaikolojia.
Watafiti wa utafiti wa mwaka 2005, walipendekeza kuwa watu wanaotumia hisia chanya au mhemko kama kujiamini, kupenda na kutumaini, wanaweza kufuata malengo yao ya juu wakiwa katika hali hizi nzuri na rasilimali kwa kuchota kutoka kwa zile zilizotengenezwa hapo awali, ambazo zilitokana kwa kuwa na athari chanya.
Unapofikiria vyema zaidi, bila shaka unajisikia vizuri zaidi. Utafiti mmoja ulichukua hatua hii zaidi, ukisema kuwa furaha inaweza kuleta mafanikio. Kwa maneno mengine mafanikio hayawezi tu kusababisha hisia za furaha lakini kinyume chake kinaweza kuwa kweli pia.
Kwa bahati nzuri, mawazo chanya yanaweza kuwa na ushawishi mkubwa sana kwa afya yako ya mwili na kiakili kutoka kwa kupunguza hatari yako ya kupata unyongovu hadi homa ya kawaida. Hii ni kulingana na kliniki ya Mayo. Faida ya kufikiri chanya ni nyingi na huathiri afya yako kwa njia mbalimbali.
Njia ya kuanza kufikiri vyema zaidi ni kuanza shughuli ambazo kwa ukawaida huibua uchanya ndani yako. Hii inaweza onekana tofauti kwa kila mtu lakini fikiria kitu kinachokuacha ujiskie mwepesi na mwenye furaha zaidi.
Nikukumbushe kwamba haiwezekani kuwaza tu mawazo chanya au kuhisi hisia chanya tu kwa hivyo weka matarajio yako kuwa ya kweli.
Akujaliaye sana.
Mashauri na mwandishi
Maureen Kemei.
Blog, kufikirichanya.wordpress.com