Kutokuwa wa kawaida.

Jamii inapenda tuwe wa kawaida sana ili uwe rahisi kwao kutudhibiti. Hivyo pale unapoenda tofauti na jamii inavyotaka uwe, unaonekana kama mtu wa ajabu na aliyepotea. Lakini hiyo ndiyo njia pekee ya kufanya makubwa na kufanikiwa.

Huwezi kufanikiwa kwa yale yaliyozoeleka kwa kufanya yale yaliyozoeleka na kuwa kama wengine wanavyotaka uwe. Utafanikiwa kwa kujisikiliza mwenyewe, kutambua utofauti wako na kuuishi. Ukijiskia vibaya pale unapokuwa tofauti na wengine. Jua huo utofauti wako ndiyo utakaokufikisha kwenye mafanikio makubwa, kama utaweza kuutumia vizuri.

Unapojua utofauti wako usiufiche wala kujionea aibu, badala yake uishi kwa kujivunia. Hata kama watu hawakuelewi, wewe ishi huo utofauti wako na waache wayaone matokeo ya tofauti unayozalisha kupitia utofauti wako.

Jamii inapenda kuwa weka watu kwenye makundi ya kazi ambayo yanaeleweka. Hivyo itakulazimisha ujitambulishe kwa kundi fulani linaloonekana.

Jamii inapenda kuwaambia watu wabobee kwenye kitu kimoja, kama lipo ndani yako kafanye. Lakini kama ndani yako unasukumwa kufanya kitu zaidi ya kimoja, basi fanya. Muhimu ni kutozima moto kubwa unaowaka ndani yako, kwani huo una nguvu ya kukuwezesha kufanya makubwa.

Ukweli ni kwamba hakuna mtu yeyote anayekujua wewe na uwezo mkubwa ulio ndani yako. Wakati mwingine hata wewe mwenyewe hujijui vizuri, kwa sababu umekuwa unahangaika na mengi na kujisahau wewe mwenyewe.

Hatua ya kuchukua, yafanye maisha yako kuwa safari ya kujitambua, kujisikiliza na kupambana kuwa bora kadiri unavyokwenda. Kwa kufanya hivyo, utaweza kufanya makubwa na ya tofauti kabisa na yale wanayofanya wengine.

Akujaliaye sana.

Mwandishi na Mshauri.

Maureen Kemei.

Blog, kufikirichanya.wordpress.com

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *