Kwa nini ni muhimu kujitambua wewe mwenyewe?

Mwenye busara ni mtu anayekubali kuwa hajui chochote – Socrates.

Mwanafalsafa wa zamani Socrates alisema : ‘jitambue’. Alimaanisha kwamba ujuzi huanza katika kujigundua. Kwake ni lazima kila mwanamume ajitahidi kupata elimu kwani hii ndiyo sharti la wema.

Utambuzi ni kujua jinsi tunavyojua. Vyanzo vingine vinasema kuwa utambuzi wa utambuzi unarejelea kujitambua kwa mtu binafsi ; yaani, ufahamu wa wewe ni nani na nini anataka kwenye maisha

Inajumlisha mambo yafuatayo :1.) kutambua uwezo na udhaifu ;2.)kuamua vitu vinavyopendwa na visivyopendwa ;3.) kujua malengo ;4.) kuelewa vipaumbele na maadili.

Kujua mambo haya huwezesha mtu mmoja kuboresha uwezo wake wa kujifunza kwa sababu humpa mtu madokezo na maelekezo kuhusu jinsi ya kuweka jitihada ya kujifunza. Kukosa kujihusisha na ugunduzi wa kibinafsi kabla ya shughuli ya kujifunza ni sawa na kwenda vitani bila bunduki na hakuna mpango mkakati wa kumshinda adui.

Kwa waelimishaji, moja ya shughuli muhimu ambazo lazima zinahitajika kwa wanafunzi ili kufanya vizuri zaidi ni kuelewa wao ni nani na wanataka nini kwenye maisha. Hii itawasaidia kubuni mbinu za kujifunza ambazo zinafaa kabisa kwa hali yao wenyewe. Kujifunza kunategemea hali mbalimbali ambazo wanafunzi huwekwa. Hakuna mtindo mmoja wa kujifunza ambao utafaa kwa wote. Mitindo ya kujifunza yenye ufanisi mkubwa pia inatofautiana kutoka hali moja hadi nyingine.

Mwalimu anapobuni njia ya kuhamisha maarifa kwa wanafunzi, uwezekano ni kwamba mawazo na dhana zinazotolewa hazieleweki, au mbaya zaidi ni kwamba zinaweza kitafsiriwa vibaya na wanafunzi. Katika hali hii uhamishaji haukufaulu. Mwanafunzi anashindwa kutambua jambo muhimu ambalo mwalimu anataka kulisistiza na lengo la kutoa maarifa kwa wanafunzi ili kuwasaidia kuboresha maisha yao halijatimia.

Uhamisho mzuri wa maarifa ni muhimu saana. Kwa kweli, hii inaweza kuchukuliwa kama kiini cha ‘kufundisha’. Uhamisho usiofanikiwa inamaanisha kuwa hakukuwa na uhamisho hata kidogo na mafundisho hayajatimiza madhumuni yake.

Kutaja Kauli nyingine ya Socrates :”ujinga ni sababu ya uovu.” kujifunza kunakusudiwa kunawasaidia wanafunzi kutoroka kutoka kwa kifungo chao cha ujinga. Ujinga ni pamoja na kushindwa kujifunza chochote. Aina nyingine ya ujinga ni pale mtu anapofikiri kwamba amejifunza jambo fulani lakini kwa hakika yaliyomo kwenye akili yake si maarifa sahihi. Hii inaweza kuhusishwa na kushindwa kwa wanafunzi kujielewa ;na wakati mwingine, kosa ni la mwalimu kwani naye haelewi kikamilifu anachowafundisha wanafunzi wake.

Ni ukweli kwamba kujifunza ni shughuli muhimu sana kwa sababu itabainisha tofauti katika maisha ya mwanafunzi. Kwa hivyo, waalimu wasichukulie taaluma yao kirahisi. Maisha ya wanafunzi yako hatarini. Waalimu lazima wawe na wasiwasi na mbinu na mikakati sahihi ambayo itawezesha uhamishaji wa maarifa sahihi kwa wanafunzi.

Akujaliaye.

Maureen Kemei.

Blog, kufikirichanya.wordpress.com

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *