Lengo kuu ni furaha.

Miaka 2300 iliyopita, Mwanafalsafa Aristotle alijumuisha kwamba watu wanatafuta furaha kuliko kitu kingine chochote. Kwamba lengo kuu la kila ambacho tunakifanya kwenye maisha yetu, ni kutegemea kupata furaha mwishoni.

Na hili ndilo linawasukuma watu kuchukua hatua mbalimbali, kuanzia kuboresha afya zetu, kuboresha mwonekano wetu, kupata fedha na hata madaraka ni kwa lengo la kutengeneza furaha kwenye maisha.

Lakini sasa tunapofanya furaha kuwa lengo la mwisho, hapo ndipo tunapojiangusha. Kwa sababu wengi wana fika mwisho wa kile wanachofikiri kitawapa furaha, lakini hawapati furaha ambayo wakifikiri wangeipata.

Hivyo njia bora ya kuipata furaha, siyo kusubiri mpaka mwisho wa kile tunachofanya, bali kutengeneza furaha wakati unakifanya.

Tafiti zinaonyesha kwamba furaha siyo kitu kinachotokea kwa bahati na wala siyo kitu ambacho fedha inaweza kununua au madaraka kumlazimisha. Furaha haitegemei matokeo ya nje badala yake inategemea jinsi tunavyotafsiri yale yanayotokea.

Kama unataka furaha ya kweli kwenye maisha, basi usisubiri mpaka mwisho wa kile kitu unachokifanya ndiyo uwe na furaha badala yake tengeneza furaha kwenye kila hatua unayopiga. Furaha inapaswa kuwa matokeo ya kile unachofanya kila siku, na siyo kusubiri mpaka ifike mwisho.

Furaha ni hali ambayo inapaswa kuandaliwa, kutengenezwa na kulindwa na kila mtu, kwa kuwa na tafsiri sahihi ya kila kinachoendelea kwenye maisha yako.

Kwa kujihusisha moja kwa moja na kila kinachoendelea kwenye maisha yako, kiwe kizuri au kibaya ndiyo tunapata furaha. Siyo kwa kukimbia au kutoroka yale yanayotokea au kujaribu kuikimbiza furaha, bali kuyaishi maisha yako kwa namna yalivyo, ndiko kunakokuletea furaha.

Hatua ya kuchukua ;jibu la kuwa na furaha kwenye maisha yako ni kujihusisha moja kwa moja na maisha yako na kupokea kila kinachokuja kwako, iwe kizuri au kibaya.

Akujaliaye sana.

Maureen Kemei.

Blog, kufikirichanya.wordpress.com

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

3 comments

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *