Kufurahia tunachofanya.

Kwa wastani, kila mmoja wetu anatumia zaidi ya theluthi mbili ya maisha yake akiwa macho, yaani anakuwa hajalala. Na zaidi ya theluthi moja ya maisha yetu tunatumia kwenye kazi au biashara ambazo tunafanya.

Hivyo, kila tunachofanya kwenye maisha yetu, kina mchango mkubwa sana kwenye hali yetu ya furaha na ubora wa maisha pia.

Kuna watu ambao wapo kwenye kazi au biashara ambazo ni nzuri sana, ambazo ukiziangalia kwa nje wewe mwenyewe unatamani ingekuwa unafanya wanachofanya. Lakini watu hao wanakuwa hawana furaha kabisa na kile wanachofanya.

Watu hawa mara zote wanakuwa na msongo wa mawazo na maisha yao hayawi bora, wanaikosa furaha kwenye maisha yao.

Kwa upande wa pili, wapo watu ambao wanafanya k+azi ambazo zinaonekana ni za hovyo na za kuirudia sana, kazi ambayo wengine wakiangalia kwa nje wanidharau na kuona haina ufahari kufanya. Lakini unakuta watu hao wakifurahia sana kazi wanayofanya, wanaifanya kwa ubora na maisha yao yanakuwa ya furaha na bora zaidi.

Wanasaikolojia wamekuwa wakijiuliza kwa muda mrefu ni nini kunachangia baadhi ya watu kupenda na kufurahia vitu ambavyo ni vya kawaida na wengine kudharau vitu ambavyo ni vizuri.

Mwanasaikolojia Mihaly Csikzentmihalyi alikuja na jibu la swali hili kwenye kitabu chake kinachoitwa flow :the psychology of optimal experience. Kitabu hiki kimeelezea kwa kina kwa nini baadhi ya watu wanafurahia kile wanachofanya wakati wengine hawafurahii.

Na pia kwa mtu binafsi, kwa nini kuna wakati unafurahia vitu fulani na vingine hufurahii kufanya. Kwa mfano umewahi kuwa unafanya kitu na ukajikuta unafurahia sana kukifanya na hutaki kuacha kabisa kukifanya, unajikuta hufikirii kitu kingine na hata muda hujui unaishaje, yaani ni kama unajikuta siku imeisha na hujui imeishaje.

Wakati kitu kingine hujiskii kabisa kukifanya, unaona kama muda hauendi na huwezi kuituliza akili yako kwa muda mfupi ili ufanye kitu hicho.

Kuchukua hatua ;hali ya sisi kuwa na furaha au kutokuwa nayo, inatutegemea, hivyo ni jukumu letu kufurahia hali zote tunazopitia kwenye maisha. Na kuhakikisha kwamba tunakuwa watu wa furaha siku zote.

Tutaangalia yale tunayopaswa kufanya ili kufurahia chochote kwenye maisha na kuwa na maisha bora zaidi.

Akujaliaye sana.

Maureen Kemei.

Blog, kufikirichanya.wordpress.com

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *