Watu wengi wanapokuwa kwenye hali ya kukosa uhuru, huwa wanapigana sana kupata uhuru,wakiamini kwamba watakapokuwa huru basi kila kitu kutakuwa rahisi kwao, watapata kila wanachotaka. Lakini huko ni kujidanganya, uhuru ni kuwajibika, kuyabeba majukumu yako na kujisimamia wenyewe.
Kwa kuwa wengi hawapendi kuwajibika, uhuru unaishia kuwa mzigo kwao na hivyo kutafuta namna ya kurudi kwenye utumwa au kuwaiga wengine. Kama kweli unataka uhuru kwenye maisha yako, lazima uwe tayari kuwajibika, bila ya kuwajibika uhuru unaotafuta hautadumu muda mrefu.
Mifano mizuri kwa mtu ambaye ameajiriwa na ajira inamkosesha uhuru, anatamani sana kwenda kujiajiri na anapochukua hatua hiyo ndiyo anagundua kwamba kujiajiri kunamtaka kuwajibika zaidi kuliko alivyokuwa ameajiriwa na kwa kuwa hakujiandaa kuwajibika zaidi, basi wengi huishia kushindwa.
Hatua ya kuchukua, hili tupate uhuru wa kweli ni lazima tuwajibike kweli kweli,kwenye kazi zetu, biashara na shughuli zote. Hakuna uhuru unaokukujia tu ni lazima kuweka kazi, hili baadae tupate uhuru wa kweli.
Akujaliaye sana.
Maureen Kemei.
Blog, kufikirichanya.wordpress.com