Mtu wa kawaida huwa anafikiria mawazo elfu mbili mpaka elf tatu kwa saa moja, na sehemu kubwa ya mawazo hayo ni mambo hasi yasiyo na faida yoyote kwa mtu.
Sasa huo ni kupoteza muda na nguvu zako. Unahitaji kutumia mawazo yako kutengeneza taswira ya mafanikio yako, baada ya kuwa umeweka malengo yako.
Pata picha ukiwa umeshakamilisha na jione jins unavyokuwa umepiga hatua baada ya kuyafikia malengo hayo. Kisha mara kwa mara ona taswira hii kwenye mawazo yako.
Muda wote mawazo yako yatawaliwe na malengo ambayo umejiwekea. Kwenye shughuli zozote zile unapaswa kuwa na mtazamo wa tayari umeshinda.
Muda wote akili yako iwe inaangalia kwenye shindi siyo litakusukuma kufanikiwa, bali pia litakuzuia usikate tamaa njiani. Huwezi kukata tamaa wakati umeshajiona mshindi.
Kwa malengo uliyojiwekea, kila wakati Pata picha kama tayari umeshayafikia malengo hayo, Pata picha upo kwenye kilele cha mafanikio, ona jinsi inavyokuwa ufahari kwako kupata mafanikio hayo, na hilo litakusukuma zaidi.
Pia, pata picha changamoto unazoweza kukutana nazo katika safari yako ya mafanikio na jione ukiwa unazivuka changamoto hizo na kuelekea kwenye ushindi.
Kumbuka kujipa taswira siyo mbadala wa kuweka kazi, kazi lazima uweke sana. Kujipa taswira ni kumiliki akili yako ili isiwe kikwazo kwako. Kwa sababu kama hutajipa mawazo ya mafanikio yako, basi mawazo ya kushindwa yatatawala akili yako.
Hatua ya kuchukua, Pata taswira ya mafanikio unayotaka kwenye maisha yako, lakini kumbuka kuweka kazi kwenye kuyafikia mafanikio hayo.
Akujaliaye sana.
Maureen Kemei
Kemeimaureen7@gmail.com