Madhara ya kusahau misingi yako.

Katika safari ya kuelekea kwenye uhuru wa kifedha na utajiri mkubwa, kujitofautisha na watu wengine ni jambo linalohitajika. Kujiwekea misingi ambayo unasimamia muda wote bila kuyumbishwa na matukio yoyote yanayotokea.

Unapoacha kuishi misingi uliyojijengea, ndipo unapoanguka. Kuishi misingi yako mwenyewe inakupa uhuru wa kuamua kufanya mambo yako kwa mpangilio mzuri, bila kufuata mkumbo.

Misingi hiyo inakupa nidhamu kubwa na kukufanya uishi maisha halisi mara zote bila kuiga au kungoja wengine wanaamua nini juu ya maisha yako. Na hapo ndipo utaweza kuzishinda hofu yoyote ile,kama hofu ya kuogopa kuchukua hatua au hofu ya kufanya kitu kipya kwenye maisha yako.

Lakini unapoacha kuishi tu misingi yako, maisha yako yanavurugika, unakosa utulivu na kuwa na hofu. Ukishajijengea misingi inayokupa mafanikio, kamwe usisahau misingi hiyo baada ya kuwa umefanikiwa.

Unapokosea kufuata misingi yako uliyojiwekea, usianze kujilaumu kwa makosa hayo, badala yake angalia ipi hatua sahihi kuchukua kisha ichukue. Haijalishi umekosea kikubwa kiasi gani, muhimu kwako ni kuanza kuchukua hatua sahihi.

Hatua ya kuchukua, jiwekee misingi unayofuata kila siku bila kuacha, na ikitokea umeacha misingi hiyo kamwe usijilaumu bali angalia ni ipi hatua sahihi kuchukua kisha ichukue.

Akujaliaye sana.

Maureen Kemei.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *