Usiogope kushindwa.

Kutoogopa kushindwa ni falsafa muhimu sana ya kufanikiwa kwenye jambo lolote ambalo mtu unafanya. Badala ya kuangalia unaposhindwa na kukata tamaa, wewe unapaswa kuendelea kufanya. Kwa sababu kadiri unavyoendelea kufanya ndivyo unavyojiweka kwenye nafasi ya kufanikiwa.

Pamoja na kwamba kuna hatua zitakazoshindwa, lakini pia kwenye hatua nyingi unazochukua, kuna ambazo zitafanikiwa. Hivyo ndivyo kanuni ya wastani ambayo ina nguvu sana katika kutufanikisha.

Kutoka kwenye kitabu cha “how i raised myself from failure to success in selling,” mwandishi Bettger anatuambia hadithi nyingi za watu waliofanikiwa huwa haziongelei yale ambayo wameshindwa. Huwa zinaweka mkazo kwenye yale ambayo wamefanikiwa.

Lakini hakuna mtu yeyote aliyefikia mafanikio makubwa ambaye pia hajapitia kushindwa kwenye hiyo safari yake. Kwa uhakika, watu waliofanikiwa wanakuwa wameshindwa mara nyingi kuliko watu ambao hawajafanikiwa.

Kinachowafanya wafanikiwe hata pamoja na kupitia kushindwa ni utayari wao wa kuendelea kufanya bila kuacha licha ya matokeo wanayokuwa wanayapata.

Kitu pekee kinachowasaidia wale wanaofanikiwa ni kutokuogopa kushindwa. Kwa mtazamo wao, waliofanikiwa hawahesabu kushindwa, bali wanahesabu ni sehemu ya juhudi ambazo wanapaswa kuweka ili kupata kile wanachotaka.

Haijalishi unafanya nini, kila vikwazo na kushindwa unakopitia siyo mwisho. Mtaji wako mkubwa ni juhudi ambazo umekuwa unaweka. Kadiri unavyoweka juhudi kubwa ndivyo unavyojisogeza karibu zaidi na mafanikio makubwa unayoyataka.

Hatua ya kuchukua :kwa ufupi , huwezi kufanikiwa bila kupitia vikwazo na kushindwa. Na pale unapopitia hali hizo, usiziangalie zikakukatisha tamaa, badala yake angalia juhudi endelevu unazoweka. Ni juhudi hizo ndiyo nafasi kubwa ya kukufikisha kwenye mafanikio unayoyataka.

Akujaliaye sana.

Mwandishi.

Maureen Kemei.

Fikrachanya.wordpress.com

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *