Chochote kinachokutisha unapaswa ufanye zaidi, Derek kwenye kitabu chake cha” Hell yeah or No. “anatuambia kuwa ana kauli mbiu mpya anayoiishi kwenye maisha yake, ambayo ni hii :chochote kinachokutisha ndiyo unapaswa kukifanya zaidi.
Anatuambia kwa miaka 30 amekuwa akiifuata kauli mbiu hiyo na imemwezesha kufanya makubwa sana.
Chochote unachotaka, ila inakutisha au kukupa hofu, ni kiashiria kwamba hicho ni kitu sahihi kwako. Hivyo usiogope na kuacha, badala yake kikabili. Hapo ndipo kwenye ukuaji na mafanikio.
Ukweli ni kwamba, unapokikabili kile kinachokutisha, hukiogopi tena. Unapata ujasiri mkubwa wa kuendelea kukifanya kwa viwango vya juu zaidi.
Mwanasaikolojoa Abraham Mascow amewahi kunukuliwa akisema :”Maisha ni mchakato endelevu wa kuchagua kati ya usalama (kwa kuhofia na kujilinda) na hatari (kwa kupiga hatua na kukua).” Chagua zaidi ukuaji kuliko hofu.
Hatua ya kuchukua ;kwa kuchagua zaidi ukuaji kuliko hofu, ndivyo unavyopaswa kuyaishi maisha yako, chochote kinachokutisha au kukupa hofu, ndiyo unapaswa kukifanya zaidi.
Akujaliaye sana.
Maureen Kemei.