Njia ya kuelekea kwenye uhuru.

Njia ya kuvuka utumwa ni kwenye kupata uhuru wa muda. Hii ni njia ya Ustoa ambao wanafalsafa kama Seneca aliamini kuwa uhuru kamili kwenye maisha ni uhuru wa muda.

Pale mtu anapoweza kudhibiti na kupangilia muda wake ndiyo anaweza kuwa na uhuru wa maisha. Kwenye kila mwanzo wa barua yake kwa Lucillus, Seneca alimsisitiza aendelee kujiweka huru kwa kuchukua udhibiti wa muda wake ambao alikuwa ameupoteza kwa muda mrefu.

Kama unapoteza muda au kama muda wako unadhibitiwa na watu wengine basi jua haupo huru. Wale wanaodhibiti muda wako ndiyo wamekufanya kuwa mtumwa wao.

Wastoa pia waliamini ni wenye hekima pekee ndiyo wanaoweza kuwa huru. Wakiamini mtu asiye na hekima huishia kusumbuliwa na hisia mbalimbali zinazomfanya asiwe huru.

Na pia Seneca anasisitiza watu wengi hawapo huru siyo wa sababu wameshikiliwa kwa lazima kwenye utumwa, bali kwa sababu wao wenyewe wameushikilia utumwa kwa lazima. Yaani hawataki kuachilia vitu ambavyo vinawanyima uhuru.

Hii ndiyo hali iliyopo sasa, ambapo japokuwa kila mtu yupo huru kimwili, kisaikolojia wengi wawejishikilia kwenye utumwa wa aina mbalimbali.

Hatua ya kuchukua ni wakati sasa wa kuondokana na kila aina ya utumwa tuliopo na kuwa huru. Kwa kuanza na kudhibiti muda wetu na kujijengea hekima ya kuweza kukabiliana na kila jambo kwenye maisha.

Akujaliaye sana.

Mwandishi wako.

Maureen Kemei.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *