Jinsi ya kuwa tayari kufanya mabadiliko kwenye maisha yako.

kwako rafiki yangu mpendwa:

Yapo mambo mabaya yanayoweza kukusukuma ukate tamaa mapema, pale unapoanza kuchukua hatua ya kubadilika.

Namna unavyofikiri kuhusu mchakato mzima wa mabadiliko kwenye maisha yako,inaweza kushawishi jinsi utakavyoendelea.

Unapaswa kuwa makini na mawazo kama hayo yanayoweza kujaribu kukupa hofu wakati unafanya mabadiliko.

Unapaswa kuwa makini na mawazo hasi kama yafuatayo;hii haifanyi kazi kwangu,hii hiwezi ikawa,ni ngumu kwangu,ni msongo sana kwangu kuachana na mazoea,ninachofanya sasa sio ngumu,hakuna haja nijaribu,kwa sababu nilijaribu kitu kama hicho mwanzoni na haikufaulu na siendani na mabadiliko vizuri.

Kwa sababu unafikiri itakuwa ngumu haimaanishi huwezi ukafanya.Mara nyingi vitu vizuri maishani zinakuja kutokana na uwezo wetu wa kuamua kuchukua hatua na kuweka juhudi.

Ikiwa unafanya mabadiliko fulani kwenye maisha yako au hufanyi, unaweza ukatengeneza utaratibu wa kufanya mabadiliko.

Unaweza ukafanya mabadiliko polepole kwenye maisha yako kwa kutumia njia yafuatayo;

Tengeneza mpango kwa yale unataka kukamilisha kwa siku thelathini zijazo.Tafuta lengo moja ambayo unataka kufokasi na ukatengeneza matarajio halisi unayotaka kuona mwezi ikiisha.

Tengeneza msimamo wa tabia unayoweza kufanya kila siku. Tafuta hata kama ni step moja kila siku itakufikisha kwenye lengo lako.

Tarajia changamoto njiani.Tengeneza namna ambavyo utaweza kukabiliana na changamoto hizo.Kufanya matengenezo mapema kutakusaidia kukaa kwenye mchakato.

Jiwekee uwajibikaji,huwa tunafanya vyema tukijiwekea uwajibikaji kwenye uendelevu wetu.Jiwekee uwajibikaji kwenye yale unapaswa kufanya kila siku.

Chunguza maendeleo yako. Amua jinsi utakavyokuwa unaangalia maendeleo yako. Kuweka rekodi ya ushindi wa kila siku itakushawishi kukaa kwenye mchakato wa mabadiliko.

Kama lengo lako ni kufanikiwa kwenye mauzo, jifunze jinsi wanaofanikiwa wanafanya aje mauzo,kisha fanya kama vile wanavyofanya.

Hatua ya kuchukua; kaa kama mtu ambaye anataka kubadilika kweli kwa kufuata mipango hizi na utaweza kuona mabadiliko polpole.

Mwandishi wako

Maureen Kemei

www.uamshobinafsi.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *