Kwa nini tunajaribu kutawala kila kitu!

Eneo la udhibiti na maisha yako.

Rafiki wangu mkubwa karibu.

Unapokabiliana na changamoto maishani mwako,je,unahisi kwamba una uwezo wa kudhibiti matokeo,au unaamini kwamba uko chini ya huruma ya nguvu za nje? Jibu lako kwa swali hili linarejea eneo lako la udhibiti.

Eneo letu la udhibiti huathiri mwitikio wetu kwa matukio katika maisha yetu na ushawishi kwenye kuchukua hatua.

Ikiwa unaamini kuwa unashikilia funguo za hatima yako,kuna uwezekano mkubwa wa kubadilisha hali yako inapohitajika.

Kinyume chake ,ikiwa unafikiri kwamba matokeo ni nje ya mikono yako,unaweza kuwa na uwezekano mdogo wa kufanya kazi kuelekea mabadiliko.

Watu walio na internal locus of control yaani eneo la udhibiti la ndani huamini kuwa wana uwezo wa kuamua kesho yao itakuwaje. Wanawajibika kwa mafanikio au kufeli kwao kwenye maisha. Wanaamini wana uwezo wa kutawala kila kitu kuanzia kwenye fedha zao hadi kwenye utajiri wao.

Eneo lako la udhibiti linaamua jinsi unavyoona hali kwa mfano ebu fikiria mtu anayeomba kazi ,ana kila kitu ,amevuzu vizuri ana uzoefu wa kazi ya kampuni hilo.

Alafu baada ya muda kidogo anapigiwa simu kuwa hakufanikiwa kupata kazi hiyo. Kama mtu uyo ana udhibiti wa nje (external locus of control). Atafikiria kuwa,”hakika wana watu ambao wamevuzu vizuri zaidi kuliko mimi,labda haikuwa kazi nzuri kwangu”.

Kama ana udhibiti wa ndani (internal locus of control) atafikiria kuwa,”sikuweza kufanya kazi nzuri inayowafurahisha,au najua naweza fanya vizuri sana,nahitaji kuongeza juhudi zaidi kwenye kujifunza kuhusu kazi hiyo na kampuni hiyo.”

Mambo mengi huathiri eneo letu la udhibiti kwa mfano yale uliyopitia ukiwa mdogo,kama ulikua kwenye familia ambayo wanapenda kufanya kazi kwa bidii, utajifunza kuamini udhibiti wako wa ndani. Kwa sababu utaamini kwamba kufanya kazi kwa bidii na juhudi kubwa ndio kila kitu kwenye maisha.

Kwa upande mwingine wa shilingi kama ulikua kwenye familia ambayo wazazi wako wanakuaminisha wakati wote kuwa “wewe si kitu,huwezi chochote,hata ukifanya nini dunia itakuonea sana’ utakuwa na udhibiti wa nje yaani external locus of control.

Yale unayopitia kila siku kwenye maisha huchangia kwenye eneo lako la udhibiti.Ukipata mafanikio ambao umeng’ang’ania sana ,utaona kuwa una uwezo wa kutawala zaidi matokeo.

Lakini ukiwa na mtazamo kwamba kila kitu unachokifanya kwenye maisha yako hakiendi,utaona kwamba huna udhibiti wowote.

Udhibiti wa ndani umeonekana kuwa ndio nzuri zaidi,unaweza ukafanya chochote ukiamini na kuweka kwenye akili yako.

Hata hivyo watu walio na nguvu kubwa ya udhibiti wa ndani wanaweza wakawa wakuu wa makampuni (high CEOs).Kwa sababu wanaamini kwenye kuleta mabadiliko.

Wauguzi pia wana udhibiti mkubwa wa ndani ,kwa sababu wanaamini kwamba wanaweza wakatibu wagonjwa na hata kupuni dawa za kuponya magonjwa mbalimbali.

Lakini pia udhibiti huu una madhaifu yake,kwa mfano unaweza jiamini zaidi kwamba unaweza ukatawala kila kitu hata yale yaliyo nje ya uwezo wa binadamu.

Mwandishi wako

Maureen Kemei.

www.uamshobinfsi.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *