Kwako rafiki yangu mkubwa, kama umekuwa ukilalamika au kuudhiwa na watu wengine kwa sababu tu ya kukukosoa kuwa hufanyi vizuri, au huwezi kitu inamaanisha umepeana nguvu zako.
Wakati wowote unaposhindwa kuweka mipaka ya kihisia na kimwili, Kuna uwekezekano mkubwa kwako upeane nguvu zako kwa watu wengine.
Huenda huwezi sema ‘hapana’ wakati jirani wako anahitaji kitu kutoka kwako. Au hutaki kupokea simu kutoka kwa rafiki yako anayependa kulalamika kila wakati, lakini unaendelea tu kupokea simu hiyo inapoitana.
Kila wakati unapoona ni ngumu useme ‘hapana’ kwa kila kitu,unapeana nguvu zako.
Kama hutachukua hatua kuhakikisha unapata mahitaji yako, utakuwa umewapa watu nafasi ya kuchukua yaliyo yako.
Kukosa mipaka ya hisia ni tatizo kubwa, kama hutaki jinsi mtu anavyokuchukua, lakini huwezi ukajitetea, unampa uyo mtu nguvu ya kutawala maisha yako.
Kadiri unavyotoa nguvu zako, ndivyo unavyopungua zaidi katika kujirekebisha.
Baadhi ya matatizo unapopeana nguvu zako ni kama yafuatayo.
Unategemea wengine waamue jinsi unavyohisi. Unapopeana nguvu zako unakuwa unategemea wengine na udhibiti kutoka nje ili kuamua hisia zako. Maisha hubadilika badilika, wakati mambo yanaenda vizuri, unajisikia vizuri, lakini yanapobadilika, mawazo, hisia na tabia zako hubadilika pia.
Unawapa watu nafasi ya kuamua thamani yako. Ukipeana nguvu zako, utakuwa mzuri tu kama utaendana na maamuzi ya wengine. Na hutapokea sifa au mrejesho wowote kuhusu yale unayohitaji.
Unaepuka kujadili shida ilipo.Ukipeana nguvu zako inaashiria kuwa hujiwezi. Badala ya kutafuta suluhisho la tatizo ya jinsi unavyoweza kujiboresha, unatafuta udhuru yasiyokuwa na mashiko ili kuhalalisha tatizo.
Unakuwa mwathirika wa hali fulani. Unakuwa msafiri kwenye maisha yako, badala ya kuwa dereva. Unaanza kusema watu wengine wanakufanya ujiskie vibaya au kukusukuma ukae kwa njia ambayo hupendi. Unalalamikia wengine badala ya kukubali uwajibikaji.
Utakuwa nyeti sana kwa kukosolewa. Utakosa fursa ya kutathmini ukosolewaji. Badala yake, utaweka moyoni yale ambayo wengine wanasema. Utapeana nguvu zako kwa maneno ya wengine badala ya yale yaliyo na tija.
Unapoteza mmalengo yako. Hutaweza kutengeneza aina ya maisha unayotaka ukipea watu uhuru na nafasi ya kukutawala. Hutajituma kwa ajili ya malengo yako vizur, ukipeana nguvu zako watu watakuvuruga kabisa hadi uachane na malengo yako.
Una ua mahusiano. Kama hutaongea wakati watu wanapokuumiza, hisia zako au unawapa uwezo wa kukunyanyasa, utakuwa unasikia uchungu juu yao.
Mwandishi wako.
www.uamshobinafsi.com
Ahsante sana Maureen kemei ,kwa somo zuri nikwel tunapaswa kutunza nguvu zetu kwa manufaa yetu nasiyo kuzigawa hovyo hovyo kwa mambo ya siyo na faida kwetu.