Kutarajia matokeo ya haraka inakufanya uachane na juhudi zako. Kama huoni matokeo yoyote moja kwa moja, utaona kuwa juhudi zako hazifanyi kazi.
Mwanabiashara ambaye amewekeza kwenye biashara yake mpya anaweza kufikiria juhudi zake hazifanyi kazi kwa sababu hakuona ongezeko wa haraka kwa mauzo.
Lakini uwekezaji wake kwenye masoko itaongeza bidhaa ichulikane ambazo zitasaidia kuongeza mauzo kwa muda mrefu.
Kuna utafiti uliofanywa kwamba tunakata tamaa sana kwenye malengo yetu haraka.
Utafiti wa mwaka 1972 ulionyesha kuwa asilimia 25 wanaacha mipango zao za mwaka baada ya wiki 15.
Baadhi ya matokeo hasi yanayoweza kutokea wakati unapotarajia matokeo ya haraka ni kama yafuatayo;
Unapata jaribu la kuchukua njia ya mkato.Kama hupati matokeo ya kutosha,unaweza fikiria mambo na kutamatisha kwa njia isiyofaa. Kazi ya kutumia njia ya mkato inaweza kuleta matokeo hatarishi.
Huwezi jitayarisha vizuri juu ya kesho yako. Ukitaka kupata kila kitu kwa sasa itakuzuia kwenye kuona mambo ya muda mrefu . Kutaka kupata matokeo ya haraka inatokana na watu kuangalia uwekezaji wao .
Watu wakiwekeza wanataka kuona matunda ya uwekezaji wao mapema,bali sio miaka 30 ijayo.
Kuwa na matarajio bila mpango nzuri inakufanya uhitimu matokeo bila kuyatafakari vyema,Ili kufikia uamuzi wa mwisho.
Mtu ambaye hajasimamia biashara vizuri anaweza kujiona kama amefeli au asiye na bahati. Kwa sababu hakupata faida, lakini kiukweli hakujipa muda ya kujifunza na kutengeneza biashara.
Huleta matokeo hasi na hisia zisizo sahihi. Kama hutafikia matarajio yako utakuwa unaumizwa moyo,kukosa uvumilivu na kuchanganyikiwa .
Ukipata hisia hasi zinazoongezeka , maendeleo yako inapunguka unajaribiwa kukata tamaa kabisa wakati ambapo ungetarajia matokeo mazuri.
Utajiingiza kwenye tabia yanayokuzuia kufikia malengo yako. Kutarajia kusikoeleweka itafanya kuwa kugumu kufikia matokeo unayoyataka.
Kwa mfano kama unataka kutengeneza keki haraka unaweza fungua lango la oven na kuangalia mara kwa mara. Kila wakati unapofungua ,unapa nafasi joto litoke, itafanya keki ichukue muda zaidi iive.
Hatua ya kuchukua, kutaka vitu yawe haraka tabia na juhudi zako zitakuzuia kabla hata hujapata kugundua.
Mwandishi wako
Maureen Kemei.