Faida 4 za kuchelewa kujiridhisha.

kutosheleza kuchelewa.

Kuchelewa kuridhika ni kipengele muhimu cha kujidhibiti unapokataa raha ya mara moja badala yake kutafuta thawabu ya muda mrefu,unajiwekea kiwango cha juu zaidi cha mafanikio kwenye vipimo mbalimbali.

Kufikia uwezo wako wote unahitajika kuonyesha umahiri wako wa kukaa kwenye hali ngumu kwa muda ,yaani uwezo wa kucheleweshwa kwa kile unachohitaji sasa ndio upate mengi mazuri baadae,hilo ni hitaji muhimu kwenye safari ya mafanikio.

Tuangalie yale watafiti wanasema kuhusu kuchelewesha kwenye kutosheka.

Kuwa na uthibiti mkubwa wa kiakili. Unapoimarisha uwezo wako wa kutafuta tuzo za muda mrefu ,badala ya usumbufu wa muda mfupi,pia utaimarisha afya yako ya akili na ustawi . Kwa utulivu huu mkubwa wa kiakili ,kukaa kwenye mchakato wa kufikia malengo ya mbali inakuwa rahisi zaidi.

Inasaidia kwenye kupata nidhamu binafsi ambayo ni muhimu zaidi kuliko kuwa na IQ ikija kwenye mafanikio darasani.

Wanafunzi wa chuo kikuu hali yao ya kuwa na kiasi inaendana sawasawa na kujiamini kwao,ufaulu wao darasani na kupunguza kwenye matendo ya uasherati na kukuza zaidi vipaji.

Kucheleshwa kwenye kutosheka kunasababisha mtu kuwa na asilimia ndogo ya msongo wa mawazo, hofu na pia sonona.

Kupungua kwa ushiriki katika tabia ya hatari. Watoto walio na hali ya juu ya kiasi wanakuwa na uchache wa magonjwa ya akili na ya kimwili. Utumiaji wa madawa za kulevya pia zinapungua,ugaidi na fedha za watu wazima zinakuwa salama.

Kama malengo yako ni kuweka akiba yakutosha Ili uende mapumziko mwakani,ama unajitahidi kuwalea watoto ambao watakuwa wanawajibika wanapokuwa wakubwa,unapaswa kuweka matarajio mazuri na yanayotimizika kwako na usiwe na haraka wa kuona matokeo ya haraka.

Hata hivyo,unapaswa ujitoe kwa malengo hayo kwa muda mrefu,hivyo utaongeza uwezekano wa kufikia mafanikio makubwa hatimaye unatimiza ndoto zako.

Mwandishi wako.

Maureen Kemei

http://www.uamshobinafsi.com/wp-admin

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *