Kwanza mdomo. Kama mdomo wako hauna break utakosana na watu wengi na watu muhimu watakukimbia.Mara nyingi ata ukiwa na akili sana huwezi ongea point kila mara,hivyo ili kutunza heshima yako hakikisha unakuwa sio muongeaji sana . Usipende kuchangia kila mazungumzo.
Pili ni omba omba. Kila mtu ana shida zake ,kama unataka watuwasikuchoke jitahidi sana uache tabia ya kuombaomba . Watu watakuchoka kama kila ukipiga simu unataka kuomba pesa, unataka kusaidiwa. Ni kweli kila mtu kwenye maisha huhitaji msaada lakini usizidi,usiwe mtu wa kusaidiwa kula mara.
Tatu uvivu. Hakuna anayependa mtu mvivu,ukiwa mvivu huwezi kuvutia watu wa maana kwenye maisha yako,sanasana utavuta wavivu yaani wenzako tu. Ukiwa mvivu pia ni ngumu kupata maendeleo hivyo utavuta umaskini kwani utakuwa hufanyi kazi kwa bidii.
Nne Uchafu. Je wewe unapenda kukaa karibu na jirani mchafu? Uchafu ni tabia ambayo husababishwa na uvivu,wengi hujitahidi kulinda usafi wa mavazi ,lakini wanapoishi ni wachafu. Wengine maeneo yao ya kazi au biashara ni uchafu tupu.
Tano kukosa msimamo. Mnakubaliana na mtu kuhusu jambo fulani,ila baada ya muda anabadilika. Watu walio na msimamo sio watu wazuri kufanya nao kazi ,hao ni wepesi sana kukuruka na pia huwa sio wawajibikaji.
Sita ni hasira. Hasira ni hisia mbaya sana ambayo inaweza kukufanya ufanye maamuzi ambayo utajutia. Hasira husababisha kutukana,kupingana,kususia,kwa vitu vidogo vya kumaliza kwa amani. Lakini ukiwa mtu wa hasira utapoteza watu wengi kutokana na ugomvi wako.
Hatua ya kuchukua, tabia zetu zinaamua ni watu Gani tuwe nao kwenye maisha,tunavutia watu wanaofanana na tabia zetu.
Tabia zako zinaamua wateja waje kwenye biashara yako au waende kwingine. Tabia pia zinaamua kazini upewe cheo Gani! Na mwisho tabia zinaamua mafanikio yako.
Wako akupendaye sana
Mwandishi Maureen Kemei
http://www.uamshobinafsi.com/wp-admin