Kama ilivyo kwa Kocha yeyote yule ambaye anakusanya mawaidha yaliyo bora na mazuri ,kwa ajili ya kukusaidia wewe ufikie kile ambacho unakitaka kwenye maisha yako.
Unapaswa pia uwe hivyo rafiki yangu kwenye safari hii ya kutafuta mafanikio. Unahitajika ujitoe vivyo hivyo kwako mwenyewe. Ona yale unayoweza ukafanya vizuri na uweke nguvu zako hapo ,chunguza eneo ambayo yanakuhitaji uboreshe na ujipe jaribio la kuwa bora zaidi.
Tafuta fursa za kujiboresha zaidi,lakini kwenye nyuma ya akili yako kaa ukijua na uelewe kwamba hutakuja kuwa bora zaidi. Unajaribu kuwa bora taratibu taratibu kwa kuzingatia njia tatu zifuatazo:
Njia ya kwanza ,chunguza tabia zako. Pata picha pale ambapo tabia zako zinashinda uwezo wako ,uwezo wa kujenga nguvu zako za akili. Kwa mfano ,kurudia kosa kisha tafuta mipango zitakazokusaidia ukae kwenye mchakato sahihi wa kujenga nguvu za akili .
Ya pili ni kuzawazisha hisia zako. Angalia wakati ambapo unajihurumia unapoogopa kufanya kitu ,unaogopa kuwa peke yako , hufurahii mafanikio ya wengine au hata unahofia kuwa hujaweza kufurahisha wengine.
Hupaswi kuruhusu hisia hizo zikurudishe nyuma,kumbuka ukitaka kubadilisha jinsi unavyohisi unatakiwa kubadilisha jinsi unavyofikiri na kubadilisha tabia zako zisizo nzuri.
Tatu ,fikiria kuhusu mawazo yako. Inakuchukua nguvu ya ziada na uwezo Ili kuelewa mawazo yako. Lakini kuwa chanya kupitiliza au hasi kupitiliza, huchangia jinsi unavyohisi na pia tabia zako na hata kuchangia kwenye nguvu zako za akili.
Chunguza kama mawazo yako ni ya kweli kabla ya kuamua ni nini unachotaka kufanya,hivyo hukusaidia kwenye kufanya maamuzi bora zaidi kwako.
Zingatia mawazo na Imani ambazo zinaweza kukurudisha nyuma,kama vile yale yanayochangia upeane nguvu zako,upoteze uwezo wako,kwenye mambo ambayo yaliyo nje ya uwezo wako,kukaa kwenye mambo yaliyopita,au kutarajia matokeo ya haraka. Badala yake badilisha hayo yote na mawazo yanayochangia kwenye kujenga mawazo chanya kwenye maisha yako.
Ni wazi kwamba hutaweza kubadilisha maisha ya kila mmoja. Ni uamuzi wa kila mmoja wetu, lakini badala ya kulalamikia watu hao ambao hawana nguvu za akili, jitahidi kuwa mfano bora kwao.
Unapaswa kufundisha watoto jinsi ya kuwa na nguvu za akili kwa sababu hawatafundishwa na dunia. Lakini jambo muhimu zaidi ni kujikaza kuwa bora zaidi kwako,na watu walio karibu na wewe wakiwamo watoto wako watagundua hilo.
Mwandishi wako.
Maureen Kemei.
http://www.uamshobinafsi.com/wp-admin