Hatua 10 za kuchukua Ili kuweza kuwa na utulivu wa mwili.

Kila tunachoweka kwenye miiili yetu na jinsi tunavyoitumia na kuhifadhika kwenye miili yetu,kunachangia sana kuwa na utulivu au kukosa utulivu.

Njia ya kwanza ni kujifunza kusema hapana . Rasilimali kama muda na nguvu ni rasilimali mbili ambazo tunazo kwa uhaba ,tunapaswa kuzitumia kwa umakini sana. Unaposema ndiyo kwenye vitu visivyo muhimu,unasema hapana kwenye yaliyo muhimu.

Njia ya pili ni kwenye kufanya matembezi. Tunapaswa kutenga muda ya kufanya matembezi Ili kuondokana na mkwamo. Matembezi pia ni njia bora ya kufanyia mwili mazoezi,na pia njia bora ya kutafakari kuhusu maisha kwa ujumla.

Njia ya tatu ni kuondokana na vitu ambavyo huvitumii. Tunapochukua hatua ya kupunguza vitu ambavyo tunavimiliki ,ndivyo tunavyotoa nafasi na nguvu kwenye yale ambayo ni muhimu zaidi kwenye maisha.

Njia ya nne ni kwenye kutafuta upweke. Kwa kujitenga na kukaa peke yako kwa muda itakupa nafasi ya kutafakari na kufikiri vizuri,kusali na pia kutahajudi.

Njia ya tano ni kuwa mtu. Kwa asili tunapaswa kupata muda wa kupumzika,muda wa kutafakari,muda wa kujua ukomo wa uwezo wetu na pia kuishi ndani ya ukomo huo.

Njia ya sita ni kwenye kupata usingizi wa kutosha. Usingizi ni riba tunayolipa kwa kuwa na maisha, hivyo kama hatupati usingizi wa kutosha maana yake hatulipi riba. Usingizi siyo anasa bali ni kitu muhimu sana kwetu kama tunataka kuwa wa mwili imara wenye utulivu.

Njia ya sapa ni kuwa shujaa . Maisha tunayoishi sasa imekuwa ya ubinafsi mkubwa,kila mtu anasumbuka na mambo yake na hataki kujua kuhusu nwenzake. Ili kuwa shujaa wa kweli tunapaswa kukataa ubinafsi na kuwa tayari kutoa mchango wetu kwa wengine,na pia kusimamia kilicho sahihi mara zote.

Nane ni kutafuta hobi. Ili mwili wetu upate utulivu ,hasa pale unapofanya kazi kwa muda mrefu , unapaswa kuwa na hobi. Ni kitu ambacho unapenda kukifanya na siyo tu unafanya kwa sababu unapaswa kufanya. Na pia siyo kwa sababu unafanya Ili wengine wakuone.

Tisa ni kutengeneza utaratibu wa kuiendesha siku. Ili kuondokana na kupoteza nguvu nyingi ya kuamka na kutafakari ufanye nini kwanza , unapaswa kupangilia siku yako vizuri. Kwenye kutengeneza utaratibu huo,amabayo unakuwa unaiendesha siku yako. Unapangilia ni muda gani utakuwa unalala na muda gani utaamka na utafanya nini na nini.

Tukio la mwisho. Ulimwengu huu sio makao yetu,tumo humu kwa muda mchache mno ,kifo ndio tukio la mwisho kwenye maisha ya kila mmoja wetu. Kifo ndio kitu pekee ambacho hatuwezi kukikimbia. Siku tuliyozaliwa ndiyo tulipewa adabu ya kifo.

Wanafalsafa wengi huwa wanasema kuwa lengo la falsafa ni kujifunza kufa. Na njia pekee ya kujifunza kufa ni kujifunza kuishi vizuri kila siku yetu. Kuuishi kila siku kama vile ndiyo siku ya mwisho wa uhai wetu.

Kuchukua hatua ya kufikiri kwa usahihi,kujiimarisha kiroho,kutafuta maana na uzuri wa maisha. Tunapoyaendesha maisha yetu tunapaswa kuuishi na kutunza miili yetu Ili isije tukafa mapema kabla ya kutimiza ndoto zetu.

Kuishi vizuri na kwa utulivu kutayafanya maisha yetu yawe bora na kifo chetu kuwa chema.

Mwandishi wako akupendaye sana.

Maureen Kemei

http://www.uamshobinafsi.com/wp-admin

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *