Kutoka katika kitabu cha ‘everyday ero manifesto ‘ mwandishi Robin anatushirikisha wakati alipokutana na Desmond Tutu, mwanaharakati wa Africa kusini aliyefanya kazi kwa karibu na Nelson Mandela katika kuikomboa Afrika kusini na kuponya mfumo wa ubaguzi.
Robin anasema kitendo cha kukutana na Desmond kilileta nguvu kubwa na ya kipekee ndani yake,kupitia yeye kuna mambo makubwa muhimu sana aliyojifunza.
Mambo hayo ni kama yafuatayo:
Kuwa jasiri kusimamia kile kilicho sahihi bila ya kujali nani anayekupinga ,lakini pia kuwa tayari kuwasamehe waliokuumiza kwa namna mbalimbali.
Kila binadamu hapa duniani ni muhimu bila kujali rangi, jinsia,dini au utaifa. Na kila mtu anapaswa kuchukuliwa kwa heshima uelewa na upendo.
Umuhimu wa kila mtu kuishi upekee ambao upo ndani yake,kuvunja minyororo ya ukomo ambayo tumejengewa na kuwa halisi ,kitu ambacho kina mchango mkubwa hapa duniani.
Kila mtu ni kiongozi hata kama hana madaraka. Asili huwa haipendi kuwepo kwa utupu, hivyo popote ulipo ,asili itakupa wajibu wa kuwa kiongozi Ili kujaza ombwe lililopo. Ni wajibu wako kuwa na maono na kuwahamasisha kuyaelewa na kujiunga na maono uliyonayo.
Sisi binadamu tuna nguvu kubwa ambayo tayari ipo ndani yetu ,ni wajibu wetu kuitambua na kuanza kuitumia Ili kuweza kufanya makubwa.
Mwandishi wako akupendaye sana.
Maureen Kemei.
http://www.uamshobinafsi.com/wp-admin