Kitu kimoja kinachodhihirisha thamani yako.

Rafiki yangu unaweza kuwa unasema utakavyo ,lakini watu wataamini zaidi kile kile unachofanya. Maneno ni rahisi,kila mtu anaweza kusema atakavyo. Lakini matendo ni magumu na hayo yanadhihirisha kweli mtu anasimamia wapi.

Kama kitu ni muhimu kwako utakifanya hutaishia tu kusema nataka hivi,nataka kufanya hiki na hiki. Kama unakitaka kitu kweli utafanya kila namna mpaka ukipate ,hautakubali kuzuiwa na chochote.

Angalia yale unayofanya ,hayo ndiyo yanaonyesha zaidi ni nini unajali . Hata kwa wengine,usisikilize wanasema nini , wewe angalia wanafanya nini . Kama maneno na matendo ya mtu vinatofautiana, wewe amini zaidi vitendo kuliko maneno.

Hivyo kwa wale ambao kila mwaka wanaema wanataka kuanza biashara ila hawana mtaji,au uwezo au muda au kingine chochote,jibu unalo hapa kuwa hawataki kuanza biashara.Wangekuwa wanataka kweli wangekuwa wameanza.

Kuchukua hatua, Ili ukubalike na uaminike katika jamii ni vizuri kuwa watu wa vitendo,watu wenye kutia bidii kwenye kila tunachokifanya. Tukifanya hivyo tutaweza kutengeneza fursa nzuri ya kukubalika na kuaminika na pia maisha yatakuwa mazuri zaidi.

Kuongea kwingi kunaleta jina ambayo sio nzuri kwenye jamii na pia watu watachoka na wewe kwa haraka. Na kibaya zaidi hutaaminika na fursa zikitokea kwenye jamii utakuwa mtu mwisho kupewa iyo fursa ,hivyo maisha yako yatakuwa magumu kidogo.

Hivyo tuweke kazi kwenye matendo zaidi kuliko kuongea. Maana maneno ni rahisi na kila mtu anaweza akaongea jinsi awezavyo,lakini matendo ni magumu na wachache sana wanaweka nguvu kwenye matendo na kazi yao.

Mwandishi wako akupendaye sana.

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *